NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ SHEHA wa Chumbageni wilaya ya Mkoani, Mgeni Othman Shaame, jioni ya leo anatarajiwa kuwaongoza wanachi wa kijiji cha Kidutani, kuzipitisha sheria ndogondogo, zitakazowaongoza wananchi hao, ili kujenga tabia njema . Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa kamati ya elimu na maadali ya kijiji hicho Machano Ali Makame, alisema jioni ya leo, kijijini hapo watakuwa na ugeni wa shehia yao. Alisema kuwa, sheha huyo pamoja na ujumbe wake akiwemo askari wa shehia, watakutana na wananchi hao, na kuzijadili kwa mara ya mwisho kanuni, hizo kabla ya kuzipitisha rasmi. Alieleza kuwa, kijiji hicho kimeamua kuanzisha kanuni hizo, ili kuwasawaidia vijana kuwaelekeza kwenye maadili mema, ili wawe raia bora wa taifa hili. ‘’Ni kweli jioni ya leo, Sheha wa Chumbageni ataungana na wananchi wa kijiji cha Kiduatani, ili kuzipitisha kanuni, ambazo zilianzishwa na wananchi wenyewe,’’alisema. Mwenyekiti wa kamati hiyo Mwalimu Saleh Abdalla Mohamed, alisem...