Skip to main content

Posts

Showing posts from August 2, 2026

JUMAZA INAUNGA MKONO MARIDHIANO VYAMA VYA SIASA ZANZIBAR

  NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@ JUMUIYA ya Maimamu Zanzibar    (JUMAZA) imesema inaunga mkono tamko la maridhiano ya chama cha CCM  na ACT Wazalendo kwani ni hatua   ya msingi katika kuimarisha  amani, umoja na maendeleo ya  Zanzibar. Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo,  Shekh Ali Abdalla Amour, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Jamatkhan Vuga mjini Unguja. Alisema jumuiya hiyo imepokea kwa faraja na furaha maridhiano yaliyotangazwa hadharani  Julai 9, katika viwanja vya Ikulu  Zanzibar mbele ya Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia  Suluhu Hassan. Aidha alisema ni vyema kwa   viongozi hao kutofanya khiyana katika  utekelezaji wa makubaliano hayo ili  kuendelea kujenga amani, umoja   na mshikamano kwa wananchi wa Z anzibar. Alieleza kuwa jambo hilo limeonesha  utayari wa viongozi kuweka mbele maslahi ya Zanzibar na wananchi wake badala ya ...

UNDP, PACSO WAWAPA DOZI YA KISHERIA WANANACHI UWANDANI, WENYEWE WAFURAHIA

    NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ MWANASHERIA wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum ‘SMZ’ Aziza Suleiman Mohamed amesema, jamii imekuwa ikifahamu udhalilishaji, unaopelekea madhara ya kimwili, bali unajumuishwa madhara ya  kingono, kihisia, kutelekezwa pamoja na kumnyima mtu usalama wake. Ameyasema hayo jana August 3, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa shehia ya Uwandani wilaya ya Chake chake, juu ya elimu iliyoandaliwa na Mwemvuli wa Asasi za Kiraia Pemba PACSO na kufanyika skuli ya Uwandani. Alisema kuwa upo udhalilishaji mbalimbali unaojumuishwa madhara ya kingono, kihisia, kutelekezwa pamoja na kumnyima mtu usalama wake. Alisema matokeo ya udhalilishaji ni makubwa kiasi ambacho, kunaweza kusababisha majaraha, kifo kuenea kwa maradhi tabia hatarishi na matokeo mabaya kwa wanaofanyiwa. Alifafanua kuwa wahanga wakubwa wanaothirika na vitendo hivyo ni wanawake, watoto na watu wenye ulemavu, hivyo ipo sheria ya Mtoto nambari 6 ya mwaka 2011,...