NA HAJI NASSOR, DODOMA WAZAZI na walezi, wametakiwa kuzungumza na watoto wao wachanga kwa lugha rasmi, zinazozungumzwa na jamii yao, kwani kufaya hivyo, ni sehemu ya kuongeza makuzi, ufahamu na utanuzi wa ubongo wao. Kwani, tafiti zimegundua kuwa, watoto hata wanapokuwa tumboni, wanauwezo mkubwa wa kusikia mazungumzo ya lugha yoyote, hivyo mara wanapozaliwa wazazi wawe nao karibu. Muwezeshaji kwenye mafunzo ya Kitaifa ya Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ‘SECD’ kutoka Mombasa Kenya Everlyne Okeyo, aliyaeleza hayo mjini Dodoma. Alisema, watoto wanakosa ukuaji mzuri wa kutengeneza ubongo wao, kwa kule wazazi kutowashughulika kuzungumza nao, wakidhani hawana uwezo wa kufahama lugha zao. Alieleza kuwa, makuzi mazuri ya awali ya mtoto, ni baina ya siku moja baada ya kuzaliwa hadi miaka minane, ambapo hapo huwa rahisi kwa wazazi na walezi, kuweke mwelekeo wa maisha ya mtoto. ‘’Wazazi waliowengi wamekua wanaanza kuweka nguvu zaidi za watoto wao, mara...