NA HAJI NASSOR, PEMBA:::- MAZINGIRA ni vitu vyote vinavyotunzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai. Vitu vyenye uhai, ni pamoja na mimea na wanyama, lakini visivyo na uhai ni pamoja na hewa, maji na ardhi. Maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho, hutegemea mahusiano mazuri kati ya watu na mazingira . KWANINI TUYAHIFADHI MAZINGIRA? Hifadhi ya mazingira ni juhudi zinazofanywa na binadamu, ili kuhakikisha dunia anamoishi usiharibiwe na utendaji wake, bali uweze kuwafaa watu wa vizazi vijavyo. Tunatakiwa tutunze mazingira, kwani tukiyachafua tutapata magonjwa ya mlipuko kama vile kipindu pindu na mengine mengi. SABABU ZA MATOKEO YA UCHAFUZI WA MAZINGIRA Binadamu ndiye anayehusika na uchafuzi wa mazingira, na maendeleo yake ya viwanda na teknolojia na ukuaji wa idadi ya watu ni sababu zingine, zilizo wazi za kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira. Katika miaka ya hivi karibuni, kwa njia hii uzalishaji wa gesi zinazochafua mazingira, uzalishaj