Skip to main content

Posts

Showing posts from October 25, 2026

BANDARI YA MANGAPWANI KUCHOCHEA UKUAJI WA UCHUMI

NA TATU MAKAME@@@@   KUKAMILIKA kwa mradi wa Bandari Jumuishi ya Mangapwani imetajwa kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa Zanzibar na Tanzania Bara, ambayo itasaidia kuimarika kwa shughuli za biashara na usafirishaji wa mizigo.   Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, Waziri wa Fedha Tanzania, Balozi Khamis Mussa Omar alisema, bandari hiyo itachochea ukuaji wa uchumi hasa usafirishaji wa mizigo.   Hata hivyo alilitaka Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ili wananchi wanufaike na huduma hizo.    "Ipo haja kwa  Shirika la Bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  kushirikiana kwa pamoja na kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa zitakazotokana na mradi huo," alisema.   Alisema, ni muhimu kwa wadau wa TRA kufuatia mradi huo na kuweka mazingira yatakayowezesha shughuli za biashara kwa wananchi pamoja na kunufaika na mr...

WADAU WA ZSSF WAPENDEKEZA UMRI WA KUSTAAFU UBAKI ULE ULE WA MIAKA 60 NA SIO 65

  IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ WADAU wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Pemba wamependekeza, kubakia umri wa kustaafu kwa watumishi kati ya miaka 55 ya hiari mpaka 60, na sio miaka 60 kwa 65, kwani wananchi wengi wanapofikia umri huo wanakabiliwa na maradhi mbalimbali, ikiwemo shinikizo la damu, kisukari na ugonjwa wa moyo ambayo humsababishia kushindwa kufanya kazi vizuri.   Walisema kuwa, rasimu hiyo ya Sheria isiangalie tu watu wachache ambao wana muonekano mzuri wa kiafya na wenye nguvu katika kipindi cha umri huo, na kuliacha kundi kubwa ambalo linapofikia umri wa miaka 60 linakabiliwa na maradhi mbalimbali, yanayowafanya washindwe kuwajibika ipasavyo katika utekelezaji majukumu yao ya kazi kwenye Ofisi.   Walitoa mapendekezo hayo wakati walipokuwa kwenye mkutano wa kukusanya maoni juu ya Mswaada wa Marekebisho ya Sheria ya Mfuko ya Hifadhi ya Jamii Zanzibar, uliofanyika Ukumbi wa Tibirinzi Chake chake Pemba, wadau hao walipendekeza kuachw...

TUZ: YAPOKEA MAONI YA WADAU PEMBA MKATABA WA UTOAJI HUDUMA

  NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@ TUME ya Utangazaji Zanzibar TUZ, imeanza kupokea maoni, ili kuimarisha   rasimu ya mkataba wa utoaji wa huduma kwa wadau wa habari, ili kujenga ukaribu na uhusiano kwa wadau hao. Akizungumza katika kikao cha kupokea maoni ya wadau kuhusu mkataba huo kwa wamiliki wa vyombo vya habari   na wadau wa huduma za utangazaji,   kilichofanyika ukumbi wa mikutano ZBC Chakechake, Afisa Utawala wa Tume hiyo Zanzibar Zuwena Mohamed alisema, maoni ya wadau yatasaidia kuwa na rasimu rafiki ya utoaji wa huduma. Alisema Tume ya Utangazaji imebaini kuwa, kumekuwepo na baadhi ya watu hawaelewi huduma zinazotolewa na Tume hiyo, jambo linalopelekea kukosekana kuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya Tume na Wadau. ‘’Tumekua tukipokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wadau wetu, hivyo tumeamua kuleta mkataba huu kwenu ili kuutolea maoni ambayo yataingizwa kwenye rasimu hapo badae yenye lengo la kuondosha malalamiko hayo pamoja na mambo mengine,’’alisema. A...