NA MWANDISHI WETU, PEMBA @@@@ WANACHAMA 25 kutoka vikundi 16 vya kuweka na kukopa katika Wilaya ya Kusini Unguja wamepatiwa mafunzo ya siku mbili ya kuchagua, kupanga na kusimamia biashara . Mafunzo hayo yalitolewa chini ya Programu ya Mashirikiano ya p amoja kwa ajili ya h aki za Watu wenye Ulemavu (CADiR) inayotekelezwa na Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Shirikisho la Jumuiya za Watu wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) na Jumuiya ya wasioona Zanzibar (ZANAB) kwa ushirikiano mkubwa na Shirika la Watu Wenye Ulemavu la Norway (NAD). Amapo jumla ya washiriki 16 wa mafunzo hayo ni watu wenyeulemavu na 9 ni walezi na wasimamizi wa Watoto wenyeulemavu , ambapi wanatarajiwa kuyafikisha maarifa haya kwa wanachama wenzao, ili kila kikundi kinufaike pamoja na kuimarisha biashara zake . Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo , Aziza Ismail ambae ni Mratibu wa program ya CADiR kutoka NAD, a li sema taasisi zinazoshirikiana katika progr...