NA HAJI NASSOR, PEMBA
SHIRIKA
la Umeme la Zanzibar ZECO, limesema mita za kisasa zinazoendelea kuwekwa juu ya
posi za nyumba ya mteja, hazina athari yoyote, kutokana na jinsi
zilivyotengenezwa.
ZECO limesema, mita hizo
zina waya maaluma wa arthing ambao unaweza kukijikinga yenyewe na mishutuko
yenye mfano wa moto kama radi, jua na hata kuzuia kuingia maji ya mvua.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi kwa njia ya simu, Afisa Mawasiliano na Huduma kwa wateja wa ZECO
Pemba Haji Khatib Haji, alisema wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya mita hizo
kupachikwa juu.
Alisema, mita hizo kukana na
mjengeko wake, zinakinga maalum ambayo hairuhusu maji kupenya wala kusambuliwa
na wadudu ambao wanaweza kupelekea athari ya mita hiyo.
Alieleza kuwa, mita hizo ni
kisasa na tayari wenzao wa Shirika la Umeme la Tanzania ‘TENESCO’ wameshaanza
zoezi hilo kwa muda mrefu na hakuna athari hadi sasa.
‘’Lazima wateja wetu na
wananchi waelewe kuwa, mita hizo hazina athari, maana zimetengenezwa maalum kwa
ajili ya kupachwa juu,’’alifafanua.
Aidha Afisa huyo, alisema
mita hizo zinakuja kuondoa shaka baina ya mteja na ZECO kwamba wapo baadhi
wamekuwa wakizichezea mita watakavyo.
‘’Wapo watalaamu mitaani,
kutokana na mita nyingi kuwa chini, wamekuwa wakizichezea na wakati mwengine kutusababishia
hasara au matatizo katika mfumo wa umeme,’’alifafanua.
Hata hivyo, alisema zoezi
hilo litakuwa la nchi nzima, ingawa kwa sasa wameanza katika maeno nyumba za
wateja zinashida ya sehemu ya uwekaji wa mitra hizo.
Awali baadhi ya wateja wa
ZECO wamelalamikia kukosa taarifa za kina juu ya zoezi hilo kwa kuwekewa mita
za umeme juu ya posi za kupokelewa waya wa umeme.
Mmoja katia ya wananchi Issa
Hassan Hamad wa Kengeja, alisema hakupata uwelewa wa kutosha wa sababu ya ZECO
kuzipachika mita za umeme juu.
‘’Nilichoelezwa kuwa ni
zeozi la lazima tena la nchi nzima, na kukabidhiwa rimoti maalum, ambayo
itakuwa na uwezo wa kuwasiliana na mita yangu,’’alieleza.
Nae mteja wa ZECO Asha Humud
Saleh wa Mtambile alisema hakujua sababu ya mita hizo kupachikwa juu, ingawa
alifahamishwa namna ya kuangalia salio na kuingiza umeme.
Hata hivyo, wateja hao wa
ZECO wameomba kupewa elimu ya kina juu ya sababu ya kufungwa kwa mita hizo juu,
jambo ambalo sio kawaida.
Mwisho
Comments
Post a Comment