NA HAJI NASSOR, PEMBA
MBUNGE wa viti maalum
nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka
wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete
Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao.
Kauli
hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara
baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya
uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando.
Alisema,
hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada
ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo.
Alieleza
kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile
viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa
na mbunge wao.
“Baada
ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia
kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’alieleza.
Katika hatua nyingine, Mbunge huyo wa viti maalum wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asya Sharif Omar, alisema, viongozi wa CCM wataendelea kutekeleza ahadi kwa wananchi mbali mbali, bila ya kujali itakadi zao.
Kuhusu
sensa ya watu na maakazi, zoezi linalotarajiwa kufanyika mwaka huu, aliwataka
wananchi wasipuuze na kushiriki kikamilifu.
“Lengo
kuu la sena hii, ni serikali kupata idadi halisi ya wananchi wake, ili sasa
ipange mipango na mikakati ya kweli, maana kinyume chake, ni kufanya kazi kwa
kubahatisha,’’alifafanua.
Hata
hivyo, amewasisitiza wananchi hao wasisite kuchangia huduma ya maji safi na
salama, ili Mamlaka ya Maji Zanzibar ‘ZAWA’ kwao iwe rahisi kurekebisha
miundombinu inapoharibika.
Kwa
upande wake, Mbunge wa Jimbo la Gando Salim Mussa Omar, alisema moja ya
vipaumbele vyake ni kuona wananchi wote wanapata huduma za lazima.
Alieleza
kuwa, huduma ya maji safi na salama ni moija wa msingi mkuu wa wananchi, katika
kufanikisha mikakati yao ya maisha ya kila siku.
“Ni
kweli, hapa kijiji cha Taifu shehia ya Kinyasini wakati napita kuomba kura,
nililalamikiwa juu ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama, na
nikawaahidi,’’alifafanua.
Alisema,
alishirikiana na wananchi pamoja na ZAWA hadi kufanikisha mradi huo, ambao sasa
wananchi kadhaa watafaidika na kusahau kero ya miaka 14.
Katika
hatua nyingine, amesema atakuwa karibu mno na ZAWA, ili kuona mradi huo haufi,
kwani kuwarejesha tena wananchi kwenye dhiki waliyokuwa nayo, ni hasara.
Hata
hivyo Mbunge huyo amesema, bado Gando mpya aitakayo haijafikia, ingawa kwa sasa
mipango na mikakati yake, ikiwemo ujenzi wa matangi ya kuhifadhia maji
yameshaanza.
Mwananchi
Hamad Nassor Hamad, alisema kazi iliyofanywa na Mbunge wao, lazima waithamini
kwani, imewafanya wazaliwe upya kwenye huduma ya maji safi na salama.
Aisha
Kombo Hassan, alisema sasa mikakati yao ya kujiletea maendeleo yamepungua
changamoto, kwani awali walilazimika kutumia maji ya kuokota.
“Ilikuwa
alfajiri kubwa, inatubidi tuamke na kufuata huduma hiyo mabondeni tunakoendesha
kilimo, na wala hayako salama, lakini leo twamshukuru Mbunge wetu,’’alieleza.
Hata
hivyo Kazija Hija Makame, alisema kazi iliyobakia sasa ni kuendelea kuilinda
miundombinu ya maji safi na salama, ili yadumu kwa muda mrefu.
Kijiji
cha Taifu shehia ya Kinyasini, Jimbo laGando wilaya ya Wete mkoa wa kaskazini
Pemba, chenye wakaazi 823, kilikosa huduma ya maji safi na salama kwa miaka 14,
na kulazimika kutumia maji ya visima vya kata.
Mwisho
Comments
Post a Comment