Skip to main content

Posts

Showing posts from October 30, 2022

BARABARA KIPAPO-MGELEMA, WAMBAA KUMALIZIKA KWA LAMI MWAKANI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA:: WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Pemba, imesema imejipanga kikamilifu, ili kuhakikisha barabara ya Kipapo- Mgemelea hadi Wambaa yenye urefu wa kilomita 9.3 inamalizika kwa kiwango cha lami, katika bajeti kuu ya mwaka 2022/2023. Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mdhamini wa wizara hiyo Pemba Ibrahim Saleh Juma, wakati akizungumza na mwandishi w ahabari hizi, juu ya maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo. Alisema, wizara imeshajipaga kikamilifu ili kuona ndani ya bajeti yake kuu ya mwaka 2022/2023, fedha zilizotengwa zinatumika na kukamilika kwa kiwango cha lami. Alieleza kuwa, kwa sasa tayari jumla ya kilomita 5.5 za barabara hiyo imeshawekea lami nyepesi ‘primer’ yenye leya tatu, ambayo ni kutoka Kipapo hadi Mgelema.   ‘’Kutoka ilipoanzia eneo la Kipapo hadi kijiji cha Mgelema, yari kumeshawekewa lami nyepsi na ambapo sasa iko tayari kuwekewa lami moto na kikokoto zake nyembamba,’’alieleza. Hata hivyo Afisa Mdhamini huyo alise...

MAHAKAMA YATAJA SABABU KUTOMSOMEA HUKUMU MWALIMU SKULI YA MADUNGU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA:::: MAHAKAMA ya maalum ya makosa ya udhalilishaji ya Mkoa kusini Pemba, iliyopo Chake chake, imelazimika kumrejesha tena rumande, mwalimu wa skuli ya Madungu msingi Chake chake Ali Khatib Makame, baada ya kushindwa kumsomea hukumu yake.   Mahakama hiyo chini ya hakimu wake Muumini Ali Juma, juzi Oktoba 31, mwaka huu ilitarajia kusomea hukumu ya mwalimu huyo, anayedaiwa kumbaka mwanafunzi wake, ingawa hakusomewa, kutokana na kutokamilika.   ‘’Ni kweli leo (juzi Oktoba 31), tulitarajia kukusomea hukumu yake, ingawa kutokana na kuwepo kwa hukumu nyingi ya kwako, bado haijamalizika kuandaliwa, hivyo utarudi tena rumande,’’alisema Hakimu.   Hakimu huyo, baada ya kushauriana na upande wa mashataka na utetezi, aliamua kulirejesha tena shauri hilo Novemba 14, mwaka huu na kusema siku hiyo itakuwa na ya kusomea hukumu.   Awali Mwendesha Mashataka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka, Ali Amour Makame, alidai kuwa shauri hilo li...

KUMBE VIMELEA VYA 'TB' VINAUWEZO KIASI HIKI.....

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: KIFUA kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza, unaosababishwa na vimelea aina ya bakteria, kitaalamu vinaitwa ‘ Mycobacterium tuberculosis’.   Vimelea hivi kikawaida havionekani kwa macho matupu, mpaka muhusika atumie kifaa maalum kinachoitwa darubini.   Ugonjwa wa kifua kikuu kitaalamu unaoitwa ‘ Tuberculosis’ TB’ ni miongoni mwa magonjwa 10, yanayosababisha vifo kwa wingi duniani kote.   Pamoja na kwamba, ugonjwa huo umeenea ulimwenguni, lakini kutokana na hali ya kiuchumi kwa nchi za bara la Afrika ulivyo, ndio nao umekuwa hatari zaidi.   Tafiti zilizofanywa na Shirika la Afya Ulimwenguni ‘WHO’ zinaarifu kuwa, inakisiwa watu milioni 10 wameugua kifua kikuu ‘TB’ duniani kote, hadi kufikia mwaka 2020, na kati ya hao watu milioni 1.5 wamefariki dunia.   Utafifi huo ukagundua kuwa, kwa Zanzibar inakisiwa kuna wagonjwa 124 katika kila watu 100,000 ambapo hii ni   sawa na wagonjwa   1,612 kwa mwaka.   ...

MWALIMU SKULI YA MADUNGU KUSUKA AU KUNYOA MAHAKAMANI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: MAHAKAMA ya maalum ya makosa ya udhalilishaji ya Mkoa kusini Pemba, iliyopo Chake chake, asubuhi ya leo Oktoba 31, inatarajia kusoma hukumu ya mwalimu skuli ya Madungu msingi Ali Makame Khatib, anayetuhumiwa kumbaka mwanafunzi wake.   Mahakama hiyo, chini ya hakimu wake Muumini Ali Juma, imefikia uamuzi huo, baada ya pande zote mbili mahakamani hapo, kufunga ushahidi wao.   Ambapo kwa upande wa utetezi, ulifunga ushahidi wake tokea Oktoba 19, mwaka huu baada ya mtuhumiwa huyo kuwasilisha mashahidi wanne, wakiwemo waalimu wa skuli ya Madungu msingi.   Ambapo katika utetezi huo, walidai kuwa mtuhumiwa hawajahi kuripotiwa skulini hapo, kuwa amekuwa na vitendo viovu, hivyo wana hakika mwalimu huyo (mtuhumiwa) hajambaka mwanafunzi wake, kama ilivyodaiwa.   Kwa upande wa mashtaka ukiongozwa wakili wa serikali Ali Amour Makame, ulifunga ushahidi wake tokea Oktoba 11, mwaka huu na Oktoba 12, mahakama hiyo ikatoa uamuzi, kuwa ...