NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa kusini Pemba, kimepiga marufuku kwa watia wa nafasi mbali mbali, kuacha kujipotisha pitisha kwa wajumbe, na kuanza kampeni za chini kwa chini, kwani wakati wake haujafika. Akizungumza na mwandishi wa habari katibu wa CCM mkoani humo, Kajoro Vyohoroka, alisema huu sio wakati kwa watia nia kujipitisha karibu na makaazi ya wajumbe na kuanza kampeni. Alisema, CCM inaomfumo mzuri wa kidemokrasia wa kuwapata wajumbe watatu, ambao ndio watashushwa chini kwa ajili ya kupigiwa kura, na sio sasa kuanza kufanya jambo lolote. Alieleza kuwa, ni marufuku kwa sasa kwa watia nia hao, kufanya jambo lolote linaloashiria kampeni ama kuingilia utaratibu wa vikao vya chama, na badala yake wawe watulivu majumbani mwao. ‘’Ni kweli kuwa, hatua ya kwanza ya kuwapata wagombea wetu kwenye uchaguzi mkuu, umeshakamilika hivyo, watia wastahamili waanze kishindo cha kuwasilimu wajumbe, huu wakati wake bado,’...