NA MUZNAT KHAMIS, ZANZIBAR@@@@ TOFAUTI na vilimo vyengine tulivyovizoea ambapo mkulima hulazimika kuchimba ardhi kwa kutumia jembe ama zana nyengine, kuweka mbegu, mmea huanza kuota na tofauti na mwani ambao hulimwa kwenye maji ya bahari. Kilimo cha mwani kilianza mwishoni mwa mwaka miaka ya 1980 hapa Zanzibar, ambapo wanaume wakiwa kwenye hatari za uvuvi wanawake walizana kuingia kwenye kilimo hicho. Hata hivyo, wanawake wengi hapo awali waliokuwa wakijishughulisha na kilimo cha mwani ni wale waliokuwa kwenye mazingira magumu wakiwemo wajane, ambao ndio waliokiona kilimo hicho kuwa mkombozi. Umaarufu wa kilimo hicho zaidi unatokana na faida zake kiuchumi na kwa sababu wakulima wengi wa zao hilo hapa Zanzibar ni wanawake, ina maanisha kwamba zao hilo limekuwa moja ya nguzo ya kiuchumi katika maisha ya akina mama Zanzibar. Makala haya yanalenga kuangalia japo kwa ufupi sana namna zao hilo linavyowanufaisha kiuchumi akina mama na namna zao hilo lilivyobadilish