NA MOZA SHAABAN, PEMBA @@@@ SERIKALI ya awamu ya nane inayoongozwa na Dkt Hussein Ali Mwinyi imetekeleza ahadi yake ya kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma kuanzia mwenzi wa Oktoba mwaka kutoka shilling laki tatu kwa kima cha chini cha mshahara hadi shillingi laki tano. Ongezeko hilo ni utekelezaji wa ahadi yake alioitoa katika hutuba yake kwa wafanyakazi wa sekta za umma alipokuwa akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei 1, yaliofanyika Kizimbani Mkoa wa Mji Magharibi Unguja. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kuthibitisha utekelezaji wa ahadi hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Dkt Haroun Ali Suleiman alisema, ongezeko la mishahara limezingatia zaidi watumishi wote na pamoja na wanaofanya kazi katika mazingira magumu. "Tupo hapa kuthibitisha kua ahadi ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kuongeza maslahi ya mishahara kwa watumishi wa umma kuanzia mwenzi huu itathibitika k...