Skip to main content

Posts

Showing posts from January 11, 2026

ZANZIBAR NA SURA YA UJUMUISHI BADO KAA LA MOTO

  NA ZUHURA JABIRI, ZANZIBAR ZANZIBAR, ni kisiwa kinachojivunia amani, mshikamano wa kijamii na historia ndefu ya kuishi pamoja. Ingawa nyuma ya taswira hii ya utulivu, kuna sura nyingine isiyoonekana mara nyingi sura ya watu wenye ulemavu, wanaoendelea kusubiri usawa wa kweli . Kwa mujibu wa takwimu rasmi, Zanzibar ina watu 167,308 wenye ulemavu, sawa na asilimia 11.4 ya wananchi wake milioni 1.89.   Hata hivyo, katika meza ya maamuzi, katika ajira rasmi, na hata katika huduma za msingi, kundi hilo, bado lipo pembeni. Ijapokuwa sheria ya Watu Wenye Ulemavu ya nambari 8 ya mwaka 2022, inahakikisha haki sawa katika elimu, ajira, afya na ushiriki wa kisiasa. Lakini kati ya maandishi ya sheria na maisha ya kila siku, kuna pengo kubwa pengo linalowaacha watu wenye ulemavu wakionekana, lakini hawasikiki. “Nimejitolea maisha yangu kupambana na ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu na kuhakikisha hatusahauliki,” anasema Salma Saadat, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake W...

BARABARA MIZINGANI-WAMBAA YAANZA UJEZNI KIWANGO CHA LAMI

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia za Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, wamesema sasa wanaelekea kuondokana na changamoto ya muda mrefu ya usafiri, kufuatia kuanza kwa ujenzi wa barabara yao, kwa kiwango cha lami. Walisema, walidumu zaidi ya miaka minane, wakiwa napita kwenye barabara iliyojaa changamoto, kwa kuwepo mashimo yenye kina kirefu, misingi isiyotarajiwa, jambo lililokuwa likiwapa usumbufu. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi shehiani humo, walisema kwa sasa, wanaelekea kusahau machofu na dhiki ya barabara chakavu, kufuatia kuanza kwa ujenzi wa kiwango cha lami. Walieleza kuwa, walikuwa wakiahidiwa na wizara husika kwamba, iko siku ujenzi wa barabara yao kwa kiwango cha lami utafanyika, ingawa hawakuamini, kutokana na kukaa kwa siku nyingi. Mmoja kati ya wananchi hao Asha Khamis Juma, alisema sasa wanaanza kuona nyota njema, kufuatia serikali kuanza kutimiza ahadi ya ujenzi wa barabara yao. ‘’Tumeshayashuhudia magari ya kampuni ya Iris Cons...