Skip to main content

Posts

Showing posts from April 19, 2026

KITUO CHA ELIMU MBADALA WINGWI CHEMCHEM YA AJIRA KWA VIJANA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@ WIZARA ya Elim una Mafunzo ya Amali Zanzibar, ni moja ya wizara tegemezi hapa Zanzibar, katika kufanikisha maendeleo ya kila siku. Wizara hii, awali ilikuwa na mfumo wa elimu ya msingi, sekondari na chuo kikuu pekee, kwa miaka kadhaa. Kisha, wizara hiyo ikaanzisha mfumo wa Mafunzo ya Amali, ambao mfumo huu uliwahusu zaidi wale, walioshindwa kuendelea na elimu ya sekondari. Na kwa wakati huo, elimu ya lazima kwa Zanzibar, iliishia darasa la kumi (F11), ingawa miaka 1980, elimi ya lazima iliishia darasa la kumi na moja (F111). Haja ya kuongeza kiwango cha elimu Zanzibar, haikuja bure bali, ilitokana na maendeleo ya kielimu ya kidunia, nah apo sasa elimu ya lazima hadi sasa kwa Zanzibar inaishia kidato cga nne. JE WALIOSHINDWA KUMALIZA ELIMU YA LAZIMA WAFANYE NINI Wizara kwa muda mrefu sasa na kama alivyowahi kusema Katibu mkuu wa wizara hiyo Khamis Abdalla Said, kuwa hakuna mtoto wa kizanzibari ambae hatopata elimu. Hapa, akaenda mbali zaidi, ...