MKUU wa mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, amesema kada ya sheria itaendelea kuwa eneo muhimu katika jamii. Alisema, kwa kulitambua hilo Serikali, iliamua kutunga sheria mahusisi ya msaada wa kisheria nambari 13 ya mwaka 2018, na kuanzishwa Idara ya Katiba na Masada wa Kisheria, ili kuwafia wananchi kuwapa elimu, ushauri na msaada wa kisheria. Alisema idara hiyo imekua ikifanya kazi kubwa katika masuala mbali mbali ya msada wa kisheria Zanzibar, ili kuona wananchi wasio na uwezo wanapata haki zao za kisheria. Mkuu huyo aliyasema hayo Mei 12, mwaka 2022 wakati akiyafungua mafunzo ya kwanza ya siku 15 kwa wasaidizi wa sheria 15 wa majimbo yote kisiwani, yanayoendelea Gombani Chake chake. Alisema kada ya wasaidizi wa sheria, inasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafahamisha wananchi hususani wa ngazi za chini katika jamii, juu ya haki zao za kisheria na namna ya kufuatilia. “Mafunzo haya ni muhimu kwenu washiriki, ili mukitoka hapa muweze kwenda kutekeleza majuku...