NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@ KWA zaidi ya miaka 15 sasa wadau wa habari wamekuwa wakipaza sauti zao kutaka sheria mpya na bora ya habari Zanzibar. Wadau mfano Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar, Baraza la Habari Tanzania (MCT), na hata ZAMECO wamekuwa wakiungana na waandishi wa habari kuhakikisha sheria moja ya habari inapatikana. Afisa Program wa uchechemuzi wa sheria za habari Zanzibar kutoka TAMWA-Zanzibar Zaina Mzee, anasema moja ya sababu ya kutaka sheria mpya ya habari, ni kuona zile mbili zilizopo zinafutwa . ‘’Ipo sheria ya Tume ya Utangaazaji Zanzibar nambari 7 ya mwaka 1997, pamoja na marekebisho yake, pamoja na ile ya s heria nambari 5 ya Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu ya mwaka 1988, ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 1997. Anasema sheria hizo, zimekuwa na vifungu ambavyo sio rafiki kwa kuimarisha uhuru wa habari, pamoja na uhuru wa kuj ieleza katika jamii. Anaeleza kuwa, pamoja na ukongwe wake sheria hizo mbili ...