NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ WIZARA ya Afya Pemba imesema, itaendelea kuboresha mifumo ya utoaji huduma na upatikanaji wa huduma za afya kwa watu wenye ulemavu, kama sheria zinavyo elekeza. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Afisa mdhamini wa wizara hiyo Pemba Khamis Bilali Ali alisema, ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata huduma bora kama ilivyo kwa wengine, wizara i ta hakikisha hospitali zinawekwa njia za kupitia watu wenye ulemavu (Ramp) ili kupita kwa urahisi pale wanapofika kufuata huduma. Alisema jambo jengine linalotekelezwa ni kutoa maelekezo kwa watoa huduma za afya kuhakikisha wanatoa kipaombele kwa watu wenye ulemavu wanapofika hospitalini, kama kanuni zinavyo eleza ili kuhakikisha watu hao wanapata haki yao ya msingi ya afya bila ya usumbufu. “Tumeweka (Ramp) pia kuna kanuni zinazo wataka watoa huduma kutoa kipaombele kwa wenye ulemavu na wizara inasimamia kwakaribu suala hili na linafanyika”, alieleza. Alisema ingawa kuna changamoto ya wakalimani ...