NA MARYAM NASSOR, ZANZIBAR@@@@ MTUHUMIWA wa kesi ya kuua kwa makusudi, inayosikilizwa mahakama kuu Tunguu Zanzibar, inayomkabili Omar Mahmoud Abdallah (36) mkaazi wa Jang’ombe Unguja, ameendelea kusota rumande, baada ya upande wa mashtaka, kushindwa kukamilisha upelelezi wa shauri hilo kwa wakati. Mara baada ya kufika mahakamani hapo, mtuhumiwa huyo akitokea rumande, Mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar Said Ali Said, alimueleza Jaji wa mahakama kuu Zanzibar kuwa, kesi iyo ipo kwa ajili ya kuanza kusikilizwa maelezo ya awali, lakini bado upelelezi wa shauri hilo haujakamilika. “Mheshimiwa Jaji leo, kesi hii ipo kwa ajili ya kusikilizwa, lakini bado hatujakamilisha upelelezi wa kesi na mashahidi, hivyo tunaomba utupangie tarehe nyingine, kwa ajili ya kusikilizwa,’’ alidai. Baada ya maelezo hayo, Jaji wa mahakama kuu Zanzibar Ali Mohamed Ali, a...