Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Wanawake (UN Women) Bi. Sima Sami Bahous amesema kazi inayofanywa na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ) kuhamasisha wanawake wengi zaidi kushiriki kwenye nafasi za uongozi ni ya kupongezwa na kuthaminiwa na kila mmoja kwa lengo la kufikia usawa wa kijinsia baina ya wanaume na wanawake. Bi Sima, ameyasaema hayo katika ofisi za TAMWA-ZNZ zilizopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja aipofanya ziara maalumu kuzungumza na uongozi wa chama hicho pamoja na baadhi ya wawakilishi wa asasi za kiraia,viongozi wa dini na wawakilishi wa vyama vya siasa kufuatia utekelezaji mradi wa wanawake na uongozi. Amesema amefurahishwa na mbinu mbalimbali zilizotumiwa na TAMWA-ZNZ katika kutekeleza mradi huo kwa kushirikisha makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii ikiwemo viongozi wa di...