NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMATI ya Maendeleo ya kijiji cha Mtega shehia ya Wawi wilaya ya Chake Chake, imeahidi kuwachukulia hatua za kisheria, wananchi wote wenye tabia ya kuchimba mchanga kwenye barabara yao, iliyoingia kijijini kwao. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Khamis Haji, alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu ya tabia iliyojitokeza ya uchimbaji mchanga na kusababisha mashimo kwenye barabara hiyo. Alisema, waligundua hilo baada ya kuitembelea barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 2.5, ambapo alisema waligundua mashimo yenye kina kirefu, ambayo yanaweza kuhatarisha uimara na uendelevu wa barabara hiyo. Mwenyekiti huyo alisema, lazima wawachukuliwe hatua za sheria, ambao watawakamata wakiichimba barabara hiyo kwa kuchukua mchanga, kwa ajili ya ujenzi. “Baada ya hivi karibuni kuitembelea barabara hii nikiwa na wajumbe wa kamati hii, tulikuta vishungu vya mchanga pembezoni mwa barabara yetu, na kwamba wapo wanaoichimba kwa maslahi yao...