TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Washindi wa tunzo za umahiri wa uandishi wa habari wa takwimu za wanawake na uongozi kujulikana leo usiku wa 25 Febuari, 2023. Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ), kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) leo Jumamosi tarehe 25 Febuari, 2023 zimeandaa hafla ya utoaji tunzo maalum za umahiri wa uandishi wa habari za takwimu zinazohusu masuala ya wanawake na uongozi Zanzibar ambayo itafanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil – Kikwajuni kuanzia saa 1: 00 usiku. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi katika hafla hiyo ambayo inategemewa kuhusisha zaidi ya watu 150. Kauli mbiu ya tunzo hizo ni “KAL...