NA HAJI NASSOR, PEMBA
MAHAKAMA maalum ya makosa
ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, hatimae imempeleka chuo cha mafunzo kwa
muda wa miaka 14, na kulipa fidia ya shilingi milioni 1, mwalimu skuli ya
Madungu msingi Ali Khatib Makame miaka (25), baada ya kupatikana na hatia ya
kumbaka mwanafunzi wake.
Hakimu
wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, kabla ya kusoma hukumu hiyo, alisema
ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, haukuacha chembe ya shaka na ulitosha
kumtia hatiani mshitakiwa huyo.
Alisema,
mtu pekee ambae anapaswa kuthibitisha kuingilia ama kutoingiliwa kwake ni
muathirika, ambapo upande wa mashtaka, ulithibitisha vyema bila ya kuacha
chembe ya shaka jambo hilo.
Alieleza
kuwa, upande wa mashataka uliwasilisha mashahidi wanne katika shauri hilo,
ambao wote walithibitisha mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na umri wa mtoto na
kuingiliwa kwake.
‘’Moja
ya eneo ambalo mashahidi walithibitisha ni umri wa mtoto kisheria kuwa chini ya
miaka 18, kukosekana kwa ridhaa ya mtoto kabla ya kuingiliwa, jambo ambalo limeishawishi
mahakama kwa kiwango kikubwa,’’alisema.
Hata
hivyo Hakimu huyo alisema, kwa upande wa daktari nae alithibitisha kuondoka kwa
uke wa mtoto huyo, ambae alipompokea kituo cha mkono kwa mkono Chake chake,
August 16, mwaka huu alithibitisha hayo.
‘’Ingawa
daktari alisema kuwa, mtoto ameshaondokewa na uke wake, lakini hakusema kuwa
ameingiliwa na nani, maana hali hiyo inaweza kuondoka kwa kuchanika au kutiwa
kitu chengine chochote,’’alifafanua.
Wakati
akiendelea kusoma hukumu hiyo, Hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma,
alieleza kuwa, mwalimu huyo, ilitbitika kumbaka mwanafunzi wake, zaidi ya mara
moja.
‘’Ilithibitika
kuwa mara moja, alimbaka kipembeni ndani ya darasa, mara nyingine maktaba na kisha
pia alifanya hivyo wakiwa ndani ya choo cha waalimu,’’alieleza.
Ilithibitika
kuwa, Mwalimu huyo wa skuli ya msingi Madungu, mara ya mwisho, kabla ya kumbaka
mwanafunzi wake, alimtaka abakie darasani, ili amkabidhi buku lake la somo la dini,
ingawa kumbe alimbaka.
‘’Mshtakiwa
anafundisha masomo ya dini ya kiislamu na uraia, na August 12, mwaka huu
alimtaka mwanafunzi, baada ya kuondoka wenzake abakie, ili amkabidhi buku lake,
jambo ambalo hakuwa na dhamira hiyo,’’alifafanua Hakimu.
Kabla
ya hukumu hiyo, Mwendesha Mastaka wa serikali Ali Amour Makame, aliiomba mahakama
hiyo, kumpa adhabu kali mshitakiwa huyo, ili iwe fundisho kwake.
Alisema,
mwalimu huyo alishaaminiwa na serikali na ndio maana, amepewa dhamana ya
kuwafundisha wanafunzi maadili mema, hivyo ikiwa ameyavunja, hatua kali zichukuliwe.
Mwanasheria
huyo alisema, jamii ilitarajia kuwa, mwalimu kama huyo, awe kioo kwa jamii
husika na kuijengea nidhamu n heshima skuli yake, wizara na serikali kwa
ujumla.
Aidha
wakili wa utetezi Suleiman Omar Suleiman, alimuomba Hakimu huyo kwanza,
kumpunguzia adhabu mshtakiwa huyo, kwa vile anafamilia inayomtegemea.
Baada
ya maombi ya pande zote mbili, Hakimu Muumini, aliyazingatia na kumtia hatiani
mshitakiwa huyo, kwenda chuo cha mafunzo miaka 14 na kulipa fidia ya shilingi milioni
1.
Aidha
haki ya rufaa imetolewa kwa upande ambao haukuridhika na hukumu hiyo, huku
upande wa utetezi ukiweka indhari ya kukata rufaa.
Mshitakiwa huyo Ali
Makame Khatib (mwalimu wa skuli ya
msingi Madungu), mkaazi wa Matuleni wilaya ya Chake chake, alimbaka mtoto
(mwanafunzi wake) mwenye miaka 11, kwa zaidi ya mara moja eneo la skuli ya
masingi Madungu.
Ambapo kufanya hivyo ni
kinyume na kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu
nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment