NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Pemba, imewatoa hofu wananchi wanaodhani kuwa, barabara zaidi ya kilomita 134, za vijijini zinazojengwa, kwamba hazitowekwa lami, na kusema kuwa jambo hilo sio sahihi. Wizara hiyo imesema, kwa azma ya serikali inayoongozwa na Dk. Mwinyi kupitia wizara hiyo, ni kuusuka kwa lami mtandao wa barabara zote zilizoingia vijijini, ili wananchi wazitumie kwa kipindi chote cha mwaka. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Novemba 28, 2024, Afisa Mdhamini wa wizara hiyo Pemba, Ibrahim Saleh Juma, alisema barabara zote , zinazoendelea na zitakazojengwa, zitawekewa lami , kama ilivyoa a hadi ya Rais wa Zanzibar. Alieleza kuwa, ujenzi huo ni maalum, kwa ajili ya kuwapa miundombinu ya uhakika wa barabara wananchi na hasa wakulima wanaoishi vijijini. Alifahamisha kuwa, kwa muda mrefu wananchi walikuwa wakipata usumbufu , kuanzia usafiri wao hadi mazao wanayoyasafirisha , kwenda s o koni. ‘’U...