NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema kama atapata ridhaa ya kutetea nafasi hiyo, ataijenga bandari ya Wete ili, iwe ya kisasa. Mgombea huyo wa Urais, aliyasema hayo jana, uwanja wa Gomabani ya kale, wilaya ya Chake chake Pemba, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni, kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, mwaka huu. Alisema, ili kuifungua Pemba hakuna budi suala la miundombinu ya bandari, ni lazim kupanuliwa, ili kurahisisha usafirishaji wa wananchi na mizigo yao. Alisema, tayari fedha zake zipo, ambazo ni mkopo kutoka Korea, na anachosubiri ni kupata tena ridhaa ya wananchi ifikapo Oktoba 29, mwaka huu, aanze kazi. ‘’Niwahakikishie kuwa, mini na Dk. Mwinyi kama mtatupa ridhaa, basi moja ya eneo ambalo kwa Pemba, tutaliangalia, ni ujenzi wa bandari ya kisasa ya Wete,’’alisema. Ahadi nyingine, ambayo Mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. S...