NA MARYAM NASSOR, ZANZIBAR@@@@ MTUHUMIWA wa kesi ya mauwaji, Khalfan Ali Abdallah( 26) amepandishwa katika kizimba cha mahkama kuu Tunguu Zanzibar ,kwa tuhuma za kuua kwa makusudi chanzo kikitajwa ni wivu wa mapenzi. Akisomewa shitaka lake hilo na Mwendesha mashtka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar, Ali Amour Makame, mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo. Mara baada ya kufika mahakamani hapo, mtuhumiwa huyo akitokea rumande, Mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar Ali Amour Makame Alimueleza, Jaji wa mahakama kuu Zanzibar kuwa, kesi iyo ipo kwa ajili ya kuanza kutajwa maelezo ya awali, lakini bado upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kumpa muda mtuhumiwa kutafuta wakili wa kesi yake. “Mheshimiwa Jaji leo (jana), kesi hii ipo kwa ajili ya kutajwa, lakini tunaomba uihairishe na kuipanga tarehe nyengine, ili kumpa muda mtuhumiwa kutafuta au kutafutiwa wakili, kwa ajili ya ...