Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA - Zanzibar kimesema ili wanawakwe wengi zaidi waweze kushika nafasi za uongozi waandishi wa habari wanawajibu wa kuripoti habari zitakazowaibua wanawake katika shughuli mbali mbali zitakazowawezesha wanawake kushika nafasi hizo. Kauli hiyo umetolewa na Mkurugenzi wa Chama hicho Dkt,Mzuri Issa alipokua akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari vijana kutoka Unguja na Pemba ambao wanaendelea kupatiwa mafunzo maalumu ya kujengewa uwezo juu ya kuripoti habari za wanawake kushika nafasi za uongozi sambamba na kuchochea uwajibikaji kwa maslahi ya Umma. Alisema kwa muda mrefu wanawake wengi wamekua wakishindwa kufikia malengo ya kushika nafasi za uongozi katika ngalizi mbalimbali kutokana na dhana potofu ya kuamini wanaume pekee ndio wanapaswa kuwa viongozi jambo ambalo linapingwa na mikataba yote ya kikanda na kimataifa. ‘’Nyinyi waandish...