NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ SHIRIKA la Ndege la Tanzania 'ATCL' limerejesha tena huduma zake za usafiri kisiwani Pemba, baada ya miaka 30. Shirika hilo limekuja kivyengine kisiwani Pemba, maana limeanza na punguzo maalum la nauli, na ili kulijua punguzo hilo, unatakiwa kuzitembeleza ofisi zao zilizopo mjini Chake chake mkabala na Ofisi ya CCM. Kwa taarifa zaidi soma hapo chini...... WAZIRI wa Uchukuzi wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Prf: Makame Mbarawa Mnyaa, amesema kuanza kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania ‘ATCL’ kisiwani Pemba, ni eneo jingine la kukifungua kisiwa cha Pemba, kiuchumi, kama ilivyokuwa ahadi ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. A meyasema hayo leo August 20, 2025 kwenye uzinduzi wa safari za ndege za shirika hilo, hafla iliyofanyika uwanja wa ndege wa Pemba na kusema zitaanzia baina ya kisiwa hicho, Unguja na Tanzania bara. Alisema ATCL, sasa litawarahisihia zaidi wananchi wa Pemba, wakiwemo wafanyabiashara, kufika safari zao kwa wakat...