NA HAJI NASSOR, PEMBA “KABLA ya kuja kwa mpango wa kunusuru kaya maskini, hali yangu ya maisha ilikuwa ya kubahatisha hasa kujipatia mlo walau wa siku, ilikua kazi,’’ Ni maneno ya mwanzo ya mlengwa huyo wa TASAF, Amina Shaaban Shamte, alipokuwa akizungumza nami, kwenye eno lake la malisho ya wanyama kijijini kwake Mgogoni wilaya ya Wete Pemba. Amina kabla ya kutuliwa na TASAF mikononi mwake, ilikuwa jambo la kawaida, kutimiza siku tatu bila ya mlo hata ule wa kumuwezesha kuishi. “Kwanza niwashukuru viongozi ambao walileta huu mpango wa kaya maskini, mfumo huu umekuwa ni mkombozi mkubwa kwetu sisi ambao tuna hali ngumu za maisha”, anasema. Bi Amina anasema, kabla ya kuja kwa mpango huo wa kunusuru kaya maskini, hakuwa na shughuli yoyote ya kujipatia kipato lakini baada ya kufikiwa na TASAF aliweza kujishuhulisha na biashara ya kuuza nazi na ndio safari yake ya kuona mwanga ilianzia. Katika kipindi hicho ambacho TASAF haijamfikia, watoto wake kwenye suala la kuso