Skip to main content

Posts

Showing posts with the label WAWILI WAFA KWA KUFUKIWA NA MAWE

WAWILI WAFARIKI WAKICHIMBA MAWE MICHEWENI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WATU wawili wamefariki dunia, baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mawe, shehia ya Mjini Wingwi wilaya ya Micheweni Pemba. Taarifa za mashuhuda zinaeleza kuwa, jana majira ya saa1:30 asubuhi watu hao, waliondoka nyumbani kwao na kwenda eneo hilo, kwa ajili ya kutafua mawe kama ilivyo kawaida yao. Mashuhuda hao, wakizungumza na waandishi wa habari, walisema wakati wapatwa na ajali hiyo wakiendelea kuchokoa mawe hayo, juu yao kulikuwa na mlima mkubwa wa kifusi. Mmoja wa manusura wa tukio hilo, Said Hamad Shoka, alisema wakati wanakata jiwe kubwa, juu yao kulikua na mapande ya kifusi, na kisha kuwafunika. ‘’Ni kweli kifusi ndicho kilichowafunika, wakati wao wakiwa chini wanachoko mawe, kwa ajili ya kokoto,’’alisema. Nae manusura Khatib Juma, alisema kama sio nguvu za Muumba kuwapa pumzi za kukimbiwa wakati kifusi kinaporomoka, idadi ya waliokufa yenge ongezeka. ‘’Wakati kifusi kinaporoka kilikuwa mbele yangu, nilitoka mbio nyingi sana...