NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MEYA wa jiji la Chake chake Hamad Abdalla Hamad, amevitaka vilabu vyingine vya mazoezi kisiwani Pemba, kuiga mfano unaofanywa na wenzao wa ‘Gombani Fitness club’ kwa kule kuwa karibu na jamii. Hayo aliyasema leo Machi 30, 2024 mara baada ya kumalizika kwa futari, iliyoandaliwa na klabu hiyo, iliyojumuisha wawakilishi wa vikundi vya mazoezi vya Pemba, watoto mayatima na waumini wengine na dini ya kiislamu na kufanyika ukumbi wa ZRA Gombani. Alisema, Gombani Fitness Club, imekuwa karibu mno na jamii, kwa kule kujumuika katika shughuli za umma kama za usafi, uchangiaji damu na futari ya kila mwaka. Alieleza kuwa, klabu hiyo haipo tu kwa ajili yakufanya mazoezi pekee, kama vilivyo vilabu vyingine, bali wanakwenda mbali zaidi, kwa kuwa karibu na jamii kivitendo. ‘’Mfano huu wa futari mlioiandaa, kuchangia kwenu damu kwenye shughuli mbali mbali za umma, kushiriki usafi ni mambo ya kuigwa na vilabu vyingine,’’alieleza. Aidha alieleza kuwa, ibada wal...