Skip to main content

Posts

Showing posts from 2024

KONGAMANO MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI, SHERIA MPYA ZANZIBAR IKO JIKONI

  NA MARYAM NASSOR, UNGUJA@@@ @ SERIKALI ya Mapinduzi   ya Zanzibar,   imesema   mageuzi ya sera na sheria za habari nchini yaendane   sambamba na kanuni   na maadili ya vyombo vya habari. Akizungumza katika kongamano la madhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari, Katibu mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab, akimuakilisha waziri wa wizara hiyo alisema hilo litafanikiwa. Alisema, Serikali   ya awamu ya nane, inafanya juhudi kubwa   ya kuweka mazingira rafiki kwa uhuru wa vyombo vya   habari nchini,    bila ya kuathiri uhuru wa mtu mwingine. Alieleza kuwa, hivyo wandishi wa habari wanatakiwa kufanya kazi zao   kwa kuzingatia sheria, weledi   na maadili,   ili kunufaika na sekta hiyo. Nae Afisa sheria kutoka Tume ya Utangazaji Zanzibar Khadija Mabrouk Hassan, alisema   rasimu ya sheria ya habari tayari inafanyiwa kazi kwa sasa   na iko katika hatua za mwisho katika afisi ya Mwanasheria mkuu kwa hatua zaidi. Alisema, sheria zilizofanyiwa k

KWA SHERIA HII UHURU WA HABARI ZANZIBAR NI NDOTO

  NA NIHIFADHI ISSA, ZANZIBAR.@@@@     WAANDISHI wa habari wanajukumu la kuendelea kufanya uchechemuzi wa mabadiliko ya sheria zenye mapungufu na ambazo sio rafiki kwa tasnia ya habari ili kutoa fursa ya upatikanaji wa sheria zilizo bora. Yamebainishwa hayo na Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar      Dkt. Mzuri Issa   nakusema kuwa     Sheria nambari 5 ya Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu ya mwaka 1988, ambayo imefanyiwa marekebisho sheria namba 8 mwaka 1997 sheria hii licha yakuwa ni kongwe imekuwa na mapungufu mengi yanayokwamisha haki na uhuru wa vyombo vya habari Zanzibar. Akizungumza katika kikao cha kujadili    mapungufu ya sheria zinazokwamisha uhuru wa habari huko katika ukumbi wa TAMWA Tunguu amesema Demokrasia sahihi hutegemea uhuru wa vyombo vya habari unavyoweza kusimamia maslahi ya jamii,     ikiwemo   uhuru wa kutoa maoni na kujieleza bila ya kuingiliwa pamoja   kusambaza taarifa na mawazo ya aina mbalimbali kwa kufuata

MADAKTARI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WAGONJWA

  IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA    MADAKTARI na wauguzi wa kituo cha Afya shehia ya Pandani wameshauriwa kuendelea kutoa huduma bora za kimatibabu ili jamii iwe na afya njema.   Akizungumza mara baada ya kukabidhi taa katika kituo hicho, Mkaguzi wa shehia hiyo Inspekta wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Khalfan Ali Ussi alisema, licha ya changamoto wanazokumbana nazo lakini hawana budi kujitolea katika kazi zao.   Alisema kuwa, ili jamii ipate maendeleo inahitaji watu wake wawe na afya njema kwa ajili ya kufanyakazi vizuri, hivyo ni vyema kwa madaktari kuendelea kutoa huduma bora kwa mgonjwa anaefika kituoni hapo kwa matibabu.   "Kwa kweli madaktari wanafanya kazi kubwa, hivyo tuendelee kujitolea kwa moyo safi ili jamii ipate huduma bora na afya njema," alisema Mkaguzi huyo.   Inspekta Khalfan aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wafanyakazi wa kituo hicho kuhakikisha kinadumu kwa muda mrefu, kwani wao ndio walengwa wa kupatiwa huduma. &qu

USHIRIKA WA WANAWAKE SHUNGI CHAKE CHAKE WAANZA KUUWAGA UMASKINI WA KIPATO

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANACHAMA wa ushirika wa ‘ twaomba kheir’ wa wanawake wa kijiji cha Chanjamjawiri shehia ya Shungi wilaya ya Chake chake Pemba, wamekopeshana mikopo minane, yenye thamani ya shilingi 800,000 katika kipindi cha mwaka jana pekee. Wapo wanachama sita, waliokopa shilingi 100,000 kila mmoja na wawili kukopa shilingi 50,000, kwa ajili ya kutimiza malengo yao mbali mbali, ikiwemo kukamilishia ujenzi wa nyumba zao. Ushirika huo wenye wanachama 15, unasema kima hicho cha fedha walichokopeshana sio kidogo kwa wao, kutokana na hali zao za umaskini wa kipato ulivyokuwa hapo awali. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mashika wa ushirika huo Sharifa Mohamed Khamis, alisema fedha hizo zilitokana na michango yao ya awali ya kila mwanachama, kujiwekea hisa ya shilingi 8,000 kwa mwezi, sawa na shilingi 2,000 kila mwisho wa wiki. Alisema kuwa, utaratibu huo ulianza tokea mwezi Septemba mwaka 2022, ambapo kwa mwezi, wanauwezo wa kukusanya shilingi 120,000 wast

WAANDISHI WATAKIWA KUANDIKA HABARI ZENYE KULETA MABADILIKO

  IMEANDIKWA NA KHAULAT SULEIMAN    WAANDISHI wa habari nchini wameshauriwa kutumia kalamu zao vizuri, ili kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.   Akizungumza katika mahafali ya pili kwa waandishi wa habari vijana (YMF) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Bima Mpirani Mjini Unguja, Mjumbe kutoka TAMWA Zanzibar Shifaa Said Hassan aliwataka waandishi hao kujitahidi katika kazi zao ili kuwaletea mafanikio yao na jamii kwa ujumla.   Alisema kuwa, wandishi wa habari ni chachu ya kuleta maendeleo katika jamii, hivyo ipo haja ya  kutumia kalamu zao vizuri kwa kuandika habari za kuibua changamoto ili zipatiwe ufumbuzi kwa kwa maslahi ya jamii na Taifa.   "Kuna waandishi wanajitahidi sana kuandika habari na tunaona zinaleta mabadiko chanya kwa jamii, hivyo tuendelee kujitolea katika kuisaidia jamii yetu ili tufanikiwe," alisema.   Aidha aliwataka waandishi hao vijana kuwahamasisha wengine pindi zinapotokea fursa za mafunzo washiriki kikamilifu, ili  kupta elimu

WARIOBA: 'VYOMBO VYA HABARI VINAJUKUMU KUELIMISHA UMMA MASUALA YA UCHAGUZI, DEMOKRASIA'

    NA MWANDISHI MAALUM, DODOMA@@@@ VYOMBO vya habari vina dhima na jukumu la kusaidia katika kuimarisha demokrasia hususan katika kuelimisha umma masuala ya uchaguzi ili waweze kushiriki kwa ukamilifu katika uchaguzi na kuimarisha demokrasia ya ushiriki wa wananchi kwa ukamilifu. Akizungumza katika kongamano la wadau wa habari na uchaguzi Tanzania lillilofanyika leo April 30, 2024,   katika ukumbi wa hoteli ya Dodoma Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba alisema kuwa nguvu ya vyombo vya habari havina budi kutumika katika mchakato wa uchaguzi tokea kujiandikisha hadi kupiga kura ili kuimarisha shughuli hizo za uchaguzi. Jaji warioba alisema kuwa bado vyombo vya habari havikufanya kazi zake kwa ukamilifu   katika chaguzi zilizopita hivyo kuna haja ya kubadilika katika vyombo vyetu vya habari ili viweze kufanya kazi zake kwa ufanisi. “Vyombo vya habari vinatoa habari sio elimu na vinajikita zaidi katika matokeo na havifanyi utafiti”, alifafanua. Jaji Warioba alisema kuwa enzi

MJUMBE BARAZA KUU TAIFA UVCCM AWAITA VIJANA UCHANGIAJI DAMU

  NA ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@  MJUMBE wa Baraza  kuu la  Taifa umoja wa Vijana CCM kusini Pemba,  Amriya Seif Saleh Amewataka vijana kuhudhuria kwa wingi katika kuchangia Damu salama  kila ifikapo muda kwani kufanya hivyo nikuondoa changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza kwa Mama Wajawazito na ajali mbalimbali zinapotokea. Ameyasema hayo leo 25/4 /2024 huko Uwanja wa Gombani Wiilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba  wakati walipokua  na zoezi  la uchangiaji Damu Salama ikiwa ni shamra shamra za maazimisho ya mika 60 ya Muungano wa Tanzania.  Alisema kua vijana ndio nguvu pekee katika kuendeleza Muungano katika nchi nao wana  uwezo mkubwa wa kuchangia Damu salama  hivyo nivyema kuhamasishana na kuhudhuria kwa wingi kwani kufanya hivyo ni umoja na mshikamano katika kuujali Muungano. "Ndugu zangu niwambieni kwa sasa changamoto ya damu imekua ni yakudumu kitaifa na kimataifa sio kuwa ni ya Tanzania pekeee bali ni yadunia mzima "Alieleza  Aidha aliwapongeza vijana wote na Wana

'CITIZEN BRIGED' PEMBA WAONESHWA WALIPO WANAWAKE WA KUANDALIWA KIUONGOZI

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ MWENYEKITI wa Bodi ya Jumuiya ya  Utetezi wa Mazingira na Jinsia Pemba  ‘PEGAO’ Alhajji-Amran Massoud Amran, amewashauri wahamasishaji jamii kudai haki zao za uongozi, demokrasia na siasa ‘Citizen bragged’ kisiwani Pemba, kuelekeza nguvu zao ngazi ya vyuo, ili kuwaibua wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi. Alisema, wanafunzi wanawake ambao wanajitayarisha kuja kuitumikia jamii, wako katika skuli za sekondari na vyuo vikuu, hivyo ni vyema kwa wahamasishaji hao, sasa kuhamia katika eneo hilo kufanya uhamasishaji. Mwenyekiti huyo wa bodi, aliyasema hayo jana, alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi juu nafasi ya wahamasishaji jamii kutoka TAMWA, namna ya kuwaandaa wanawake kuwa viongozi katika nafasi mbali mbali. Alisema, wanawake walioko ngazi ya elimu ya sekondari na vyuo vikuu, ndio tegemeo kubwa kwa jamii, hivyo ikiwa watawezeshwa mapema, kuingia katika nafasi za uongozi, itakuwa rahisi kwao, baada ya kumaliza masomo. ‘’Kwanza nipongez