NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amedhamiria kwa vitendo kuleta maendeleo ya kiuchumi kisiwani Pemba. Na ndio maana, anachukua juhudi mbalimbali kuhakikisha wananchi wa Pemba, wanakuwa na maisha bora kiuchumi, kwa kuendelea kuwapelekea miradi ya kimaendeleo ya kimkakati. Lengo ni kuona kwamba, kila mwananchi anajiajiri na kuajiriwa kupitia fusra za kiuchumi, ambazo zinaendelea kuletwa na Dk. Mwinyi katika kila sekta. Hayo ni ya kujivunia katika kisiwa hiki, kwani kinaenda kufunguka na kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wake. Moja ya miradi mikubwa ambayo itakuza uchumi wa wananchi kisiwani Pemba, ni ujenzi wa bandari za kitaifa ambazo zitawaingizia kipato wananchi, kwa namna moja ama nyingine na kupata maendeleo. Katika ahadi zake Dk. Mwinyi alizoziweka kwa wananchi kwa ajili ya kukuza kipato chao, ni ujenzi wa Bandari ya Shumba Mjini, iliyoko wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba. Ba...