NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAZAZI na walezi wenye watoto wao skuli ya sekondari ya Connecting Continent ya Mgogoni wilaya ya Chake chake, wamesema wameridhishwa na juhudi binafsi za waalimu, katika kuwafundisha wanafunzi skulini hapo. Wakizungumza kwenye mkutano maalum uliofanyika skulini hapo, wenye lengo la kupokea matokeo ya muhula wa kwanza, wazazi na walezi hao, walisema kutokana na ugumu wa wanafunzi ulivyo, wanaridhishwa na juhudi zao. Walisema, wengi wao wamekuwa wakikosa muda wa kuwauliza watoto wao juu ya maendeleo ya elimu, lakini waalimu hao, wamekuwa wakibuni mbinu za kuwaendeleza wanafunzi. Wazazi hao walieleza kuwa, kwa muhula huu kwanza, wameridhishwa na matokeo hayo, ambayo kwa yale ya darasa la 12, kama yengekuwa ndio ya mitihani ya taifa, kusingekuwa na mwanafunzi aliyefeli. Mmoja kati ya wazazi hao Omar Mjaka Ali, alisema kama sio juhudi za waalimu hao na mbinu mbali mbali za kuwalazimisha wanafunzi kusoma, matokeo ya muhula wa kwanza, yasingekuwa maz...