NA NIHIFADHI ISSA, UNGUJA@@@@ NI kawaida kwa watoto wa kike wakifikia umri kuanzia miaka 10, kubaleghe na kutokanana na maumbile siku hizo huanzia tatu (3) h adi saba (7). Kiutaratribu watoto hutakiwa kwenda skuli kuanzia siku 20 hadi 22 kwa mwezi mmoja lakini watoto wa kike hususan walioko vijijini, huenda skuli siku 15 hii hutokana na kuingia kwenye kawaida yaao na kukosa taulo za kujisitiri. Zanzibar yenye watu wapatao milioni 1.8 huku idadi ya vijana ikiwa ni Zaidi ya 600,000 inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa elimu ya afya na hedhi salama kwa wanawake Sharon Robert akiwa Mkurugenzi wa taasisi ya 'holding hands foundation' alifanya utafiti mwaka 2019 na kugundua kuwa, watoto wakike wanaoishi nje ya mji wanakosa kwenda skuli siku 84 kwa mwaka, katika ya siku 180 wanazotakiwa. Akiwa mwanamke na kiongozi kwenye taasisi yake Hii ilimfanya Sharon kuanzisha kampeni ya kukusanya taulo za kike na kuwapa wasichana bure maskulini. Sharon alianza ugawaji wa ta