NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANUFAIKA wa sadaka ya nyama ya Ng’ombe, zaidi ya 189 wa shehia za Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, wamepongeza hatua ya jumuiya ya udhu-hiya ya shehia hizo, kwa kukamilisha bila ya kasoro, zoezi la ugawaji wa sadaka hiyo. Walisema, wamefakiniwa kupata nyama hivyo kwa ajili hya kukamilisha mlo wa sikukuu, tena kwa wakati, jambo ambalo walijiona sawa na wingine, wenye uwezo wa kifedha. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, kwa mashatri ya kutochapishwa majini yao, mara baada ya kupokea sadaka hiyo, walisema walipatiwa wastani kilo 1.5, ambayo wingi wao walipata na sikukuu ya pili. Walisema, uwepo wa Jumuiya hiyo, kwa miaka mitatu mfululizo sasa, imekuwa ikiwahakikisha kupata kitoweleo, jambo ambalo kama sio sadaka hiyo, wapo wanaokula dagaa kavu ama samaki siku hiyo. Walisema, hatu hiyo imekuwa ikiwarahisishia maisha walau kwa siku mbili za sikukuu, jambo ambalo hujiona ni sawa na wingine wenye uwezo. ‘’Kwa hakika, juzi nilipokea...