Na Muandishi wetu Zanzibar@@@@ Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (WAMM) Mhandisi Dkt Mngereza Mzee Miraji amesema Mpango wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Zanzibar 2022-2027 wenye lengo la kuimarisha sekta ya maji na kumaliza tatizo la maji safi na salama Zanzibar alianzisha kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo mbali mbali. Mhandisi Dkt Mngereza aliyasema hayo jana katika hafla iliyoandaliwa ya kumkabidhiwa Tuzo ya Kifahari ya VIP Global Water Change Maker, Mhe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Husseini Mwinyi iliyofanyika jana Ikulu Zanzibar. Alisema katika kipindi ulichoteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini alichukuwa juhudi mbali mbali za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama, kwa kukutana na Mashirika ya Kimataifa ya Misaada ikiwemo JICA, USAID, BPI, Banks ikiwemo AFDB, wawakilishi wa balozi mbalimbali ikiwemo UK, EU, JAPAN n.k. Alielezea kwamba hivyo Wizara ya Maji, Nishati na Madini (WMNM...