NA ZUHURA JUMA, KU@@@@ WANAWAKE wametakiwa kuacha tabia ya kuweka vitu kwenye sehemu za siri, kwani wanaweza kuathiri mfumo mzima wa viungo vya uzazi. Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa chama cha Waandishi Tanzania (TAMWA) Mkanjuni Chake Chake Pemba, Mratibu wa Tume ya Ukimwi Pemba Ali Mbarouk Omar alisema, kuna baadhi ya wanawake huweka vitu katika sehemu zao za siri, jambo ambalo ni hatari kwa afya ya uzazi. Alisema kuwa, ni vyema wakawa wanafika hospitalini na vituo vya afya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili ikiwa wamepata matatizo waweze kupatiwa matibabu na sio kuweka vitu ambavyo vinaweza kuwapatia madhara zaidi. "Kuna baadhi yao huweka vitu kama wanajitibu baada ya kupata magonjwa ya kujamiiana na kuna wengine wanaweka vitu hivyo kwa urembo, haya yote hayafai kwa sababu wanaweza kuathirika katika mfumo wa kizazi," alisema Katibu huyo. Aidha, akielezea kuhusu maambukizi ya magonjwa ya kujamiiana alisema, pia yanasababisha kuathiri kiza...