Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MICHEZO

MICHEZO NI AFYA: WAZIRI PEMBE

NA MWANDISHI WETU, UNGUJA@@@@ W aziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka wananchi kujiunga katika michezo mbali mbali ili kuimarisha afya zao pamoja na kuepukana na maradhi yasiyoambukiza. Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa uekaji jiwe la msingi katika Mradi wa ujenzi wa viwanja vya Michezo midogo midogo iitwayo "Michezo kwa Maendeleo (Sports for Development) katika viwanja vya Mwera Regeza Mwendo Wilaya ya Magharib A. Unguja. Waziri Pembe alifahamisha  kwamba hata viongozi wa dini na wataalumu wa Sekta ya Afya wamekua mstari wa mbele katika kuihamasiha jamii kufanya mazoezi au kujiingiza katika michezo mbali mbali ambapo hatua hiyo itasaidia kuimarisha afya na kuijiepusha na maradhi yasiyoambukiza ikiwemo kansa, kisukari na shindikizo la damu. Aidha alisema pia michezo ni ajira na sehemu ya kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hasa kwa vijana wa jinsia zote, kwani michezo inawasaidia kujiepusha na v...

MWAKILISHI CUP CHAMBANI YAZINDULIWA, NADHAF YATUPWA NJE

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ TIMU ya soka ya Nadhaf ya Wambaa, imetupwa nje kwa matuta na timu ya Mkaa, kwenye michauano ya kuwania kombe la Mwakilishi wa Jimbo la Chambani, baada ya kutoshana nguvu kwenye dakika 90. Mchezo huo uliovuta hisia za wingi, ulikuwa wa ufunguzi, ulipigwa uwanja wa Wambaa, ambapo wanacheza kwa mtindo wa mtoano, na bingwa ataondoka na kitita cha shilingi milioni 1, kutokwa kwa Mwakilishi huyo. Wakati wanaume hao wakishindwa kutambiana kwenye dakika za kawaida, hatua ya kupigiana mikaju ya penalti, ilifanyika na timu ya Nadhaf, ikipoteza mkwaju mmoja, na wenzao kundoka na yote mitano. Kabla ya ngarambe hizo, Mwakilishi wa Jimbo la Chambani Bahati Khamis Kombo, alisema huo ni mwanzo, lakini kuna mashindani makubwa zaidi ya ngazi ya shehia yanakuja. Alisema, mashindani ya msimu huu yenye zaidi ya timu 12, ni madogo na mshindi amepanga kupata shilingi milioni 1, ingawa hayanyokuja mshindi ataondoka na shilingi milioni 5. Alieleza kuwa, wame...