NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani
Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa
wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘Mkapa’
mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba.
Watuhumiwa wengine walioanza maisha
mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar
miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘Makababu’ miaka 29, wote
wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba.
Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani
hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua
kwa maksudi Said Seif Kombo.
Ilidaiwa mahakamani hapo na
Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis
akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja
wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi.
Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa
pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchana na
saa 11:00 jioni, katika eneo la Machaomane wilaya ya Chake chake Pemba.
Ilidaiwa na Mwendesha mashtaka
huyo kuwa, kufanya hivyo ni kosa kinyume na vifungu vya 189 na 190 vya sheria
nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar, iliyopitishwa na baraza la Wawakilishi.
Mara baada ya mwendesha mashtaka
huyo kumaliza kazi ya kuwasomea maelezo ya tuhma zinazowakabili, Jaji Ibrahimu
wa mahakama kuu Zanzibar, aliwauliza wathumiwa hao, ikiwa wameelewa kosa lao.
‘’Mtuhumiwa nambari moja Anuwari
Mussa Omar hadi mtuhumiwa nambari nne Yassir Mohamed Juma, jee mumemsikia
Mwendesha mashtaka na mumemuelewa,’’aliwahoji Jaji Ibrahim.
Kwa kila mmoja na kwa wakati wake,
walimueleza Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim kuwa, wameyasikia na kuyafahamu vyema
maelezo ya kosa lao, ingawa walipoulizwa kuhusu kukubali, walikana kutenda kosa
hilo.
‘’Mheshimiwa ni kweli
tumeyafahamu maelezo ya kosa letu, lakini tunaiomba mahakama yako tukufu, itupe
dhamana ya juu tuhma tunazokabiliana nazo,’’aliomba mtuhumiwa nambari mbili Yassir
Mussa Omar ‘Makababu’.
Ombi ambalo Jaji huyo wa mahkama
kuu, alilipinga akisema kifungu cha 151 cha sheria Mwenendo wa makosa ya Jinai,
nambari 7 ya mwaka 2018, inapinga kutoa dhamana kwa kosa linalowakabili.
‘’Sheria inapinga vikali makosa
ya ubakaji, kuingilia maharimu, kubaka kwa kundi, uhaini, wizi wa kutumia silaha,
kupatikana na dawa za kulevya kiwango kikubwa na kuua kwa maksudi, kutoa dhamana,’’alifafanua
Jaji huyo.
Hata hivyo watuhumiwa hao,
waliieleza mahakama hiyo kuu kuwa, wanaewakili katika kesi yao hiyo, ingawa kwa
jana hakuweza kufika mahakamani, kutokana na sababu mbali mbali.
Jaji Ibrahim, kisha aliighairisha
kesi hiyo, hadi Novemba 30, mwaka huu na kuutaka upande wa mashtaka,
kuwasilisha mambo mawili siku hiyo, ikiwemo ushahidi wa maadishi na kufanyike
kwa usikilizsaji wa awali ‘PH’ kabla ya kuanza kwa kesi ya msingi.
Wakati huo huo, Jaji Ibrahim
Mzee Ibrahim, aliwaambia watuhumiwa hao kuwa, kwa mujibu wa sheria za Zanzibar,
kama watatiwa hatiani, adhabu yao ni kunyongwa hadi kufa.
Mwisho

Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.
ReplyDeleteMwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.
Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.
Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.
Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.
Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
dawnacuna314@gmail.com