Skip to main content

Posts

Showing posts from April 24, 2022

MWAMBE PEMBA: CHILDREN FORCED TO A LIFE OF STONE CRUSHING

  By HAJI NAASSOR, PEMBA   It is about an hour-and-a-quarter drive from Chake Chake town to Mwambe village in Mkoani District in the Southern Region of Pemba Island within Zanzibar country.   The village of Mwambe is located in a rocky area but is more fertile than the surrounding villages. It has three shehias, known here as Jombwe, Mwambe and Mchakwe.   The village has a population of 17,525,(2012 census) half of them children. Its people survive on agriculture growing beans for local consumption, and citrus and bananas to sell.   It has its own primary and secondary schools and a health centre that provides various medical services.   Besides, agriculture, the villagers are also engaged in fishing, stone crashing and mining. Since Mwambe is rocky, most people, especially the elderly and children, are involved in quarrying stone for sale.   The stone crashing business has forced many children to abandon school to earn money ...

ANAYEDAIWA KUMLAWITI MTU MWENYE ULEMAVU WA AKILI PEMBA, APATA UZIWI GHAFLA MAHAKAMANI

  NA FATMA HAMAD, PEMBA HAKIMU wa mahakama Mkoa Wete, Mwendesha mashtaka, Karani, na askari wa mahakama, wamepigwa na butwaa baada ya baba mzazi wa mtuhumiwa wa ulawiti, kudai mtoto wake ni kiziwi. Awali mtuhumiwa huyo alikuwa ni mzungumzaji mzuri, wakati kesi yake ikiendeshwa  mahakamani hapo  kabla ya kuondolewa kwa madai ya kudanganya umri. Ilibainika kuwa wazazi wa kijana huyo mwenye miaka 19, anaedaiwa kumlawiti kijana mwenzake mwenye ulemavu wa akili na kisha kupandishwa katika mahakama ya mkoa B Wete,  Febuari 13, mwaka huu ingawa kesi yake iliondolewa mwezi Machi mwaka huu baada ya kudaiwa kudanganya umri. Ndipo mahakama ya mkoa ‘B’ ilipompandisha kwenye kizimba chake na kusomewa upya shtaka lake, kama mtu mzima, ingawa baba mzazi  kabla ya mtoto wake [mtuhumiwa] kujibu lolote, alidai kuwa ni kiziwi. Hoja ya mzazi huyo, ilichukua takriban dakika mbili mahakamani hapo, ikijadiliwa baina ya hakimu, mwendesha mashtaka na baba mzazi, juu ya ulemavu...

ABDALLA HUSSEIN WA PEMBA, ULEMAVU MCHANGAYIKO HAUKUWA UKUTA KUPATA ELIMU

  NA FATMA HAMAD, PEMBA ABDALLA Hussein Rashid, ni kijana mwenye ulemavu wa mchanganyiko, sasa yuko darasani, akijumuika na wenzake kusaka haki yake ya elimu. Hakuna aliyefikiria kwamba, kijana huyo engefikia darasa la kumi (FII) skuli ya sekondari Kinyasini, maana changamoto ya mwendo, ukosefu wa mkalimani yote ameyavaa. Abdalla miaka 18, alizaliwa akiwa na mguu mmoja, huku akiandamwa na uziwi na ulemavu wa matamshi, ambapo mama yake mzazi hakuwa na tamaa ya kupata elimu kwa mtoto wake. SAFARI YA MAISHA YA ABDALLA Baada ya kuzaliwa miaka 18 iliyopita kijijini kwao Kwale Gongo Wete Pemba, mama mzazi alianza safari ya kila hospitali, ili kuhakikisha tatizo la mguu linapona. “Nilifika na mwanangu hospitali ya Unguja, baada ya kuzimaliza za Pemba, ingawa kisha, akiwa ni miaka mitatau alianza kutumia mguu wa bandia,’’anaeleza mama yake. Mama yake Abdalla, bibi Time Kombo Juma ambae huyo ni mtoto wake wa wanne , anasema safari ya mtoto wake, ilikuwa ni ya kukata tamaa zaid...

KONGAMANO LA PPC. WAANDISHI PEMBA WAONESHWA NJIA YA KWENDA VIJIJINI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba, wameshauriwa kuongeza bidii ya kuibua changamoto, zinazowakabili wananchi hasa walioko vijijini, ili sauti zao ziwafikie wenye mamlaka kwalengo la kutatuliwa. Hayo yalielezwa na wanakongamano la kujadili uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari na maadili kwa waandishi wa habari, kwenye kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya waandishi wa habari Pemba ‘PPC’ kupitia Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania ‘UTPC’ na kuwashirikisha waandishi wa habari wa Unguja na Pemba na wadau lililofanyika Gombani Chake chake. Walisema, licha ya kazi kubwa inayofanywa na waandishi hao, lakini sasa waelekeze nguvu zao zaidi vijijijini, ambako wananchi wanaoishi maeneo hayo, hawana msemaji wa shida zao. Mdau wa habari Said Mohamed, alisema wananchi walioko vijijini wamekuwa na ukosefu wa taarifa nyingi na kukosa baadhi ya huduma, hivyo waandishi wanayonafasi ya kuwasaidia. Nae Msaidizi Katibu wa Mufti Zanzibar, Sheikh Said Ahmad...

‘PMTCT’ HUDUMA MWAFAKA YA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO

    NA HAJI NASSOR, PEMBA HUDUMA ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ‘PMTCT’ ni huduma ambayo inawalenga akinamama wajawazito na wenza wao.   Huduma hii ilianzishwa, baada ya kuona kuwa asilimia 90 ya watoto chini ya miaka 15, wanaoishi na virusi vya Ukimwi inatokana na maambukizo kutoka kwa mama zao na asilimia 10 iliyobakia, ndio ambayo inatokana na sababu nyengine kama kusaidiwa damu na kubakwa.   Inakadiriwa vifo vya watoto chini ya miaka 15, vinavyotokana na virusi vya Ukimwi katika dunia ni 610,000, ambapo kati ya hivyo vifo 550,000 vimetokea katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania Zanzibar.   Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, ni moja kati ya njia kuu zinazosababisha kuenea kwa kasi ya   maambukizi virusi vya Ukiwmi.   Maambukizi hayo hutokea katika nyakati tofauti kama vile, wakati wa ujauzito, wakati wa uchungu na kujifungua, wakati wa kipindi cha kunyonyesh...