NA ZUHURA JUMA, PEMBA JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limemkamata kijana Hemed Omar Ali mwenye umri wa miaka 21 mkaazi wa Konde Chanjaani baada ya kupatikana na misokoto 60 ya dawa za kulevya aina ya bangi yakiwa nyumbani kwake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Sadi Khamis alisema, mtuhumiwa huyo amekamatwa Febuari 6 mwaka huu majira ya saa 9:30 jioni huko nyumbani kwake Konde Chanjaani Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba alipatikana na misokoto 60 ya bangi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kamanda huyo alisema, mtuhumiwa huyo ni maarufu kwa uuzaji wa madawa ya kulevya, hivyo Jeshi la Polisi limemshikilia baada ya kufanya operesheni katika maendeleo mbali mbali ya Mkoa. “Pamoja na Jeshi la Polisi kufanya msako katika maeneo yote ya Mkoa, lakini walikuwa hawajafanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo, kwa bahati nzuri tulimkamata na tunaendelea mahojiano”, alieleza Kamanda huyo. Kamanda Sadi alieleza kuwa, upelelezi wa kesi hiyo unaen...