NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmshauri kuu ya CCM taifa Khamis Hamza Chilo, amesema wateule waliopewa ridhaa na chama hicho, wanatosha kulibadili jimbo la Mtambile kimaendeleo. Chilo, aliyasema hayo Septemba 27, 2025 uwanja wa mpira Kengeja jimbo la Mtambile, wilaya ya Mkoani, kwenye uzinduzi wa kampeni kwa nafasi ya ubunge, uwakilishi na udiwani wa jimbo hilo. Amesema, CCM haijawi kufanya kosa katika kuteua wagombea, iwe ngazi ya udiwani, uwakilishi, ubunge na urais, kwani huwa tayari wameshaandaliwa kiutumishi. Alieleza kuwa, wananchi wa Jimbo la Mtambile, wahakikishe kura zao ikifikapo Oktoba 29 mwaka huu, wanawapa kura za ndio wagombea hao, ili kuja kuwalipa maendeleo. Chilo alifahamisha kuwa, wagombea wote hawana shaka, na suala la kushirikiana na wananchi, katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2025/2030. ‘’Mimi nawahidi wananchi wa Jimbo la Mtambile kuwa, wagombea mlioletewa sio maji taka, ni wapambanaji, wapiganaji na wenye uchu wa maendeleo,’’alifa...