NA HAJI NASSOR, PEMBA MTUHUMIWA wa ubakaji, Sabour Juma miaka 47 mkaazi wa Chanjaani wilaya ya Chake chake, ameiambia mahkama ya makosa ya udhalilishaji ya mkoa wa kusini Pemba iliyopo Chake chake kuwa, muda aliyodaiwa kuwa amebaka, alikuwa kwake akipiga msuwaki. Alidai kuwa, maelezo ya mashahidi kuwa majira ya asubuhi alimuingiza mtoto wa miaka 11 ndani ya choo cha nyumbani yake sio sahihi, kwani muda huo alikuwa nje ya nyumba akipiga msuwaki ‘ akisugua meno’ . Aliyadai hayo mbele ya mahakama hiyo, chini ya Hakimu Muumini Juma Ali, wakati mtuhumiwa huyo aliyekuwa akiongozwa na wakili wake Suleiman Omar, akijitetea, baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao. Alidai kuwa, familia ya mtoto huyo inachoyo naye na imemtengenezea mazingira ili kumshitaki na kumfungisha, na wala hakumumbuki kumbaka mtoto huyo. ‘’Sikumbuki kumbaka mtoto huyo wa miaka 11, aliyekuja kutoa ushahidi mahakamani hapa, bali wamenitengenezea zengwe kwa njia ya...