NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ HAKIMU wa Mahkama ya Mkoa Wete, Zuwena Mohamed Abdul-kadir, amemuhukumu kwenda chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka minne, mshitakiwa Ali Mbarouk Suleiman mwenye (18) mkaazi wa Konde Chanjaani, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuvunja nymba usiku na kuiba. Mshitakiwa huyo ametiwa hatiani kwa makosa ya kuvunja nyumba na kuiba Simu moja aina ya Sumsung, yenye thamani ya shilingi 138,000 kwa kukisia mali ya Said Mohamed Salim. Aidha Hakimu huyo alieleza kuwa kosa la kwanza la kuvunja nyumba usiku atatumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa mika mitatu, na kosa la pili la kuiba simu atumikia kwa muda wa mwaka mmoja. Mbali na adhabu hiyo, pia alitoa agizo la kurejeshwa simu kwa mmiliki ambapo, hapo awali wakati wa kuiendesha kaesi hiyo, ilikua ni kielelezo cha ushahidi mahkamani hapo. Mwendesha Mashtaka wa serikali Mohamed Ali Juma, alieleza kuwa kwa vile Mahkama imemuona na hatia mshitakiwa huyo, ni vyema kutoa adha...