NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WATUMISHI wapya wa umma kisiwani Pemba, wametakiwa kuzingatia dhana ya uzalendo na kuifanyiakazi, kwani ndio msingi mkuu wa kufanikisha majukumu yao ya kila siku. Hayo yameelezwa na Afisa kutoka Chuo cha Utawala wa Umma ‘IPA’ Zanzibar tawi la Pemba Nuhu Abubakar, wakati akiwasilisha mada ya mageuzi katika utumishi wa umma, kwa watendaji wapya kutoka taasisi mbali mbali wakiwemo wa ZAWA, uliofanyika ukumbi wa Manispaa ya Chake chake. Alisema, suala la uzalendo ni jambo kubwa katika kufikia lengo la taasisi husika, na sio kwa mtumishi kufikiria maslahi yake binafsi na kuwasahau wingine. Alieleza kuwa, watumishi waliowengi wamekuwa hawako vizuri kwenye eneo hilo, jambo ambalo huwapa changamoto wananchi wanaokwenda kutafuta huduma kwenye taasisi za umma. Alifahamisha kuwa, moja ya msingi mkuu wa uzalendo la kuipenda kwa dhati nchi, wananchi wake, utamaduni na kulinda rasilimali za umma kwa gharama yoyote. ‘’Uzalendo pia unajumuisha matumizi mazuri ya muda wa...