Skip to main content

Posts

Showing posts from May 22, 2022

SUCCESSFUL COMBINED SURGERY AT ABDALLA MZEE PEMBA HOSPITALI

  BY HAJI NASSOR, PEMBA::::::: OCTOBER 25, 2021 was a memorable day for Dr. Wang Juan, an obstetrician and gynecologist at the First Affiliated Hospital of Soochow University and a member of the Chinese Medical Team in Zanzibar. She had barely worked at Abdulla Mzee Hospital on the Pemba Island for one month when she encountered acomplicated case. Although she had an experience on the case before her arrival on the islands, she was still shocked by the complexity of the illness of her patient, a 21-year-old mother from Matele Chake Chake. The patient had been leaking urine for nearly seven months with a foul smell which made her so embarrassed that she always remained in her house. According to the Assistant Director of Abdulla Mzee Hospital and Head of Obstetrics and Gynecology, Dr. Aboud, the patient had delivered a healthy child by cesarean section five years ago. Seven months ago she expected her second child with a great joy but the baby died during childbirth due to sho

KESI YA TUHMA DAKTARI KUMBAKA MTOTO MARA TATU PEMBA KUNGURUMA TENA LEO MAHAKAMANI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::::: MAHAKAMA ya Mkoa Wete, leo itaendelea tena na shauri la ubakaji linalomkabili, daktari Is-haka Rashid Hadid, wa Kituo cha Afya Gombani, baada ya wiki iliyopita kupelekwa rumande. Leo, Mahakama hiyo maalum ya makossa ya udhalilishaji, chini ya Hakimu Ali Abdur-haman Ali,inatarajia kuwasikiliza mashahidi wa upande wa mashtaka, ambapo awali ilidaiwa upelelezi umeshakamilika. Mtuhumiwa huyo ambae ana makosa manne, matatu ni kudaiwa kumbaka mtoto mwenye 16 na la pili ni kumtorosha kutoka kwenye himaya ya wazazi wake. Awali akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Juma Mussa , alidai kuwa, mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto huyo, ambae yuko chini ya uangalizi wa wazazi wake. Alidai kuwa, baina ya Aprili 21, mwaka huu mtuhumiwa huyo alimtorosha mtoto huyo, kutoka nyumbani kwao Gombani wilaya ya Chake chake mkoa wa kusini na kumpeleka nyumbani kwake Kangagani wilaya ya Wete. Ambapo baada baada ya kumtorosha, usiku

WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA WATUNUKIWA VYETI, KISHA WAPEWA NENO

  NA MWANDISHI WETU, PEMBA::____------ JANA Mei 26, 2022, wasaidizi wa sheria kutoka majimbo 18 ya uchaguzi kisiwani Pemba, wamemaliza na kisha kutunukiwa vyeti vyao, baada ya kumaliza mafunzo ya siku 15 ya wasaidizi wa sheria. Aliyekabidhi vyeti hivyo, kwenye hafla iliyofanyika Gombani Chake chake, alikuwa Afisa Mdhamini Afiri ya Rais, Katiba, Sheria, Utamishi na Utawala Bora Pemba, Hali Ali Khamis. Kwenye hutuba yake, aliwataka wasaidizi hao wa sheria, kwenda kuisadiai jamii, ili kupunguza majanga kama ya udhalilishaji, dawa za kulevya, migogoro ya ardhi na ndoa. Hata hivyo aliwataka wasibweteke na elimu ya awali ya sheria walioipata, na badala yake, wabuni mbinu za kujiendeleza ili kupanua wigo, wa utoaji msaada wa kisheria. Aidha aliipongeza Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, kwa kuendelea kuijengea uwezo wa kisheria jamii ya Zanzibar. Mkurugenzi wa Idara hiyo Zanzibar Hanifa Ramadhan Said, alisema pamoja na kumalizika kwa mafunzo hayo ya aw

ANAYEDAIWA KUMPA UJAUZITO MWANAFUNZI KENGEJA AENDELEA KUSAKWA

    NA HAJI NASSOR, PEMBA JESHI la Polisi Mkoa wa kusini Pemba, linaendelea kumtafuta, Khamis Ali Khamis ‘Diri’ wa kijiji cha Ukunda shehia ya Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, aliedaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa skuli ya Kengeja wilayani humo. Jeshi hilo limesema, mtuhumiwa huyo aende atakako na ajifiche kwenye msitu mkubwa kiasia kigani, lakini mwisho wa siku, atatiwa mikononi na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, kujibu tuhuma hizo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kamada wa Polisi mkoani humo Richard Tadei Mchomvu, alisema baada ya kutokea tukio hilo, mwaka juzi, alituma askari wake kumtafuta kisiwani Unguja, alikokimbilia bila ya mafanikio. Alisema kwa vile mtuhumiwa huyo alijua kuwa ameshafanya jinai, kwa kumpa ujauzito mwanafunzi huyo miaka 16, aliamua kukimbia, ingawa kwa sasa wanashirikiana kwa karibu mno na Jeshi la Polisi la mikoa yote ya Unguja, kwa ajili ya kumtafua. Alieleza kuwa, kwa sasa mitego imeshawekwa kila kona, na taarifa za mtuhumiwa huyo

MSEMO AWAONESHA CHOCHORO WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA KUFIKA MBALI

                                                                           NA HAJI NASSOR, PEMBA NAIBU Mkuu wa skuli ya sheria Zanzibar ‘Zanzibar school of law’ kitengo cha taaluma, Msemo Mavare amewataka wasaidizi wa sheria kisiwani Pemba, kujiendeleza na kuwa wanasheria kamili, mara watakapomaliza mafunzo yao ya awali. Alisema, bahati ya kuingia kwenye usaidizi wa sheria ni mwanzo, hivyo ili isiwe mwisho, lazima wajiewekee mpango wa kujisomea sheria zaidi hapo baadae. Naibu huyo aliyasema hayo Gombani Chake chake Pemba, wakati akizungumza na wasaidizi wa sheria tarajali, kwenye mafunzo ya siku 15 yanayoendelea, ambayo yameandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Zanzibar. Alisema, wapo wanasheria na mawakili hapa Zanzibar, ambao mwanzo wao, walianzia kuwa wasaidizi wa sheria, na wamepanua wigo wa kutoa huduma zaidi kwa jamii. Alieleza kuwa, kada ya sheria, imekuwa tegemeo kubwa jamii ya watu maskini na wale wasiokuwa na uwelewa wa kujua misingi ya haki zao kisheria