Skip to main content

Posts

Showing posts from April 23, 2023

WADAU HAKI ZA WANAWAKE PEMBA: WATAJA YANAYOWAKOSESHA HAMU KUDAI HAKI ZAO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ IMETAJWA kuwa, wanawake wanapohaingaikia hudumza za kijamii kama vile maji safi na salama, huduma za afya ya uzazi, elimu ya lazima hupoteza mwelekeo wa kudai haki zao za kisiasa, demokrasia na uongozi. Hivyo, mamlaka husika zimeombwa kuimarisha huduma hizo kwa haraka, katika vijiji mbali mbali kisiwani Pemba, ili kuhakikisha kundi la wanawake, linafikiwa na huduma hizo kwa ukaribu. Ushauri huo umetolewa leo April 27, 2023 na wadau wa haki za wanawake, kwenye mkutano wa siku moja, wa kusikiliza changamoto na ufumbuzi wake, zinazowakabili wanawake kutodai haki zao, zilizoibuliwa na wahamasishaji jamii, waliomo kwenye Mradi wa kuwahamasisha wanawake kudai haki zao, unaoendeshwa na TAMWA, PEGAO na ZAFELA na kufanyika Chake chake. Walisema, wanawake wanayo haki ya kuwa viongozi katika maeneo kama ya jimbo, kwenye jamii, serikali na hata kwenye asasi za kiraia, lakini kutokana na kukabiliwa na changamoto za utafutaji wa huduma za kijamii, hukosa kutilia m

SIRI YA 'WABAKAJI' KUACHIWA HURU PEMBA, Utetezi wa waliobakwa huwaokoa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA WATUHUMIWA wengi wa makosa ya ubakaji wa watoto wa kike kisiwani Pemba huachiwa huru baada ama kesi kumalizikia nje ya mahakama au waliobakwa kuwatetea mahakamani, imefahamika. Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa gazeti hili kwa kufuatilia mwenendo wa kesi mbali mbali kisiwani humo, umepata ushahidi wa jinsi mabinti wenye umri chini ya miaka 18 waliopata ujauzito wakiwa shuleni, walivyotoa ushahidi mahakamani kwamba hawakubakwa bali walikwenda wenyewe kwa waliowabaka. Mmoja wa watoto waliopewa mimba wakiwa wadogo lakini wakaenda mahakamani kutoa ushahidi kuwa, hawakubakwa ni Hamida Issa (sio jina lake halisi), ambaye wakati akipata mimba alikuwa anasoma kidato cha pili katika skuli ya Sekondari Piki. “ Mahakamani nilisema sijabakwa nilimfuata mwenyewe, kwa sababu sitaki kesi wala sitaki afungwe, sijabakwa bali nilimfuata mwenyewe na nimeridhia, sikulazimishwa na ndio maana sikutaka kutoa ushahidi mahakamani kwa sababu sitaki afungwe,” anasema binti huyo

KHADIJA ALI WA CHIMBA: MNUFAIKA WA TASAF ALIYEJIKUSANYIA SHUNGU YA MIRADI, MBIONI KUJENGA NYUMBA YA KUDUMU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KHADIJA Ali Mohamed 45, wa Chimba Micheweni Pemba, sasa ana mtaji wa zaidi ya shilingi 700,000, anayo matofali 500 na kiwanja, biashara ya mitumba nchini Kenya. Mpango wake huo, ni zao la ule mpango wa kunusuru kaya maskini, unaosimamiwa na TASAF tokea mwaka 2014, ambapo kila baada ya miezi mwili, hujipatia ruzuku kati ya shilingi 30,000 hadi shilingi 44,000. Ijapokuwa mlengwa mmoja na mwengine hutofautiana upatikanaji wa ruzuku hiyo, lakini zipo fedha za msingi (lazima) ambapo kila mlengwa, hupata shilling 20,000. Anakiri kuwa, mpango ya kuingizwa kwenye utaratibu wa TASAF, kwake ulikuwa sahihi, kwani hapo kabla, alikuwa akiishi kiwango cha shilingi 5000 kwa mwezi. KABLA YA KUINGIA TASAF Kwake mlo wa siku, hakuwa na hakika nao, kutokana na kutokuwa na hata njia moja, ya uhakika ya kujiingizia kipato, licha ya kutegemewa na watoto wake wanne wakati huo. “Asubuhi nikiamka, ilikuwa najiuliza kwanza nisuke makuti ya mnazi niuze nipate kiamsha ki