Skip to main content

Posts

Showing posts from January 4, 2026

WANACHAMA ‘MCT’ WAIFANYIA MAREKEBISHO KATIBA YAO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA RAIS wa Baraza la Habari Tanzania MCT, Jaji Mstaafu Bernad Luanda, amewataka wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa wanachama wa baraza hilo, kutoa michango yao ya kina, ili kupata katiba mpya, ya baraza hilo. Aliyasema hayo leo Januari 8, 2026 wakati akifungua mkutano mkuu huo, kwa njia ya kielektroniki ya ‘ZOOM’, uliowanganisha wanachama kadhaa hai. Alisema MCT inawategemea mno wanachama hao, katika kulipeleka mbele baraza hilo, na kwa kuanzia ni lazima, kuwa na katiba inayokwenda na wakati. ‘’Niwaombe sana wanachama nyinyi hai wa MCT, leo kutoa maoni yenu, ambayo naamini, yatakuwa ndio dira ya kupata katiba mpya,’’alifafanua. Katika hatua nyingine, Rais huyo wa MCT aliwatakia kheir ya mwaka mpya wanachama wake wote, na kuwataka kuutumia vyema, katika kufanikisha malengo yao. Akiwasilisha uchakataji wa maoni kuelekea katiba mpya ya MCT, mjumbe wa sekretariet Mwanzo Lawrence Milinga, alisema moja ni kutaka kuipa hadhi ya kipekee ofisi ya MCT iliyo...

INSPEKTA KHALFAN AWAPA AKINAMAMA MITUNGI YA GESI

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA @@@@ MKAGUZI wa shehia ya Pandani Wilaya ya Wete, Inspekta wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Khalfan Ali Ussi amesema, katika kuwaunga mkono Marais kwenye suala la matumizi ya nishati safi ya kupikia, ameamua kutoa majiko ya gesi wananchi, ili kuwaondoshea usumbufu wanaoupata. Alisema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi wamekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia na kuwezesha upatikaji wa gesi kwa urahisi na kwa bei nafuu, hivyo katika kuliendeleza hilo, ameona ni vyema kuwaunga mkono marais hao kwa kuwasaidia wananchi kuwapatia Nlnishati hiyo. Akizungumza mara baada ya kukabidhi majiko hayo kwa akimama wa kaya masikini kwenye shehia za Pandani, Mlindo na Mjanaza, Inspekta Khalfan alisema kuwa amewapatia majiko hayo ili waweze kutumia nishati safi ya kupikia ambayo itawarahisishia katika shughuli zao za kila siku...