NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANACHAMA wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Chake chake kichama, wamekamilisha uchaguzi wao mkuu, baada ya kuwapata viongozi wapya, watakaokiongoza chama hicho, kwa miaka mitano ijayo. Katika uchaguzi mkuu huo, umemrejesha tena kwenye nafasi ya Katibu, aliyewahi kuwa Mwakilishi wa majimbo ya Vitongoji na Wawi wakati huo, Saleh Nassor Juma, baada ya nafasi yake kukosa mpinzani. Ambapo katika uchaguzi huo, uliofanyika Gombani Chake chake Pemba, alijizolea kura 65, kati ya kura 73 zilizopigwa, huku kura mbili zikiharibika na kura sita zikimkataa. Aidha Msimamizi wa uchaguzi huo Rashid Ali Abdalla, alimtangaaza Yussuf Salim Khamis, kuwa ndie Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, baada ya kupata kura 39 na kumshinda mpinzake Mohamed Juma Khatib aliyepata kura 34. Katika uchaguzi huo, ulimchagua Khadija Ali Abeid kuwa Mshifa fedha wa Mkoa wa Chake chake kwa kura 36, baada ya kumuangusha mgombea mwenzake, Khadija Anuwar...