Skip to main content

Posts

Showing posts from March 29, 2026

WANANCHI PEMBA, WAMPA TANO DK. MWINYI KWA HUTUBA YA UJENZI WA AMANI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa mkoa wa kusini Pemba, wameipongeza hutuba ya uzinduzi wa mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2026, iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi. Walisema, hutuba hiyo ilitoa mwelekeo wa umoja, mshikamano, upendo miongoni mwa wananchi wa Tanzania, jambo linalofaa kuungwa mkono. Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa mwenge huo, jana uwanja wa michezo Gombani, walisema hutuba imewakumbusha watanzania wajibu wao, kwa maslahi mapana ya taifa. Mmoja kati ya wananchi hao Ali Ameir Haji wa Mchangamdogo, alisema hutuba hiyo kama wananchi waliifuatilia kwa makini, basi ni darasa tosha wa ujenzi wa amani. Alieleza kuwa, hutuba nyingi anazozitoa Dk. Mwinyi kwenye hafla kadhaa za kitaifa, huwa na mwelekeo mpana, ingawa hiyo ya kwenye uzinduzi wa mwenge wa uhuru, imeongezeka mara dufu. ‘’Kwa hakika hutuba hiyo, ilijaa kila kitu mfano, imehamasisha upendo, nidhamu, umo...

ANGALIA HAFLA YA UZINDUZI WA MWENGE WA UHURU KITAIFA MKOA WA KUSINI PEMBA MWAKA 2026

 

DK. MWINYI KUZINDUA MWENGE WA UHURU ASUBUHI HII UWANJA WA GOMBANI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, asubuhi ya leo April 2, 2026, anatarajiwa kuwa mgeni, rasmi katika uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, utakaofanyika, uwanja wa michezo Gombani Chake Chake Pemba. Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Rashid Hadid Rashid, kwa vyombo vya habari, ilieleza kuwa, tayari maandalizi yote yameshakamilika kwa shughuli hiyo ya kitaifa. Taarifa hiyo ilieleza kuwa, Dk. Mwinyi ataingia kwenye kitabu cha kumbukumbu kwa zoezi hilo, ambapo kwa mara ya kwanza, lilifanyika zaidi ya miaka 10 iliyopita kisiwani humo. Mkuu huyo wa mkoa katika taarifa yake, ilifafanua kuwa, Dk. Mwinyi atawahutubia wananchi watakaohudhuria, pamoja na kuzindua rasmi mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, kwa mwaka 2026. Alieleza kuwa, wananchi watakaohudhuria kwenye zoezi hilo la kitaifa, kabla ya Dk. Mwinyi kufanya uzinduzi huo, watashuhudia burudani kadhaa uwanjani hapo. Alisema, m...

UNAIFAHAMU KAULIMBIU YA MWENGE WA UHURU WA MWAKA HUU?

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ……..MWENGE wa uhuru ni chombo cha kitaifa. Baada ya taifa la Tanzania kupata huru, kilianzisha chombo hicho, kikiwa na malengo kadhaa ndani yake. Kwa wakati huo, taarifa zinaeleza ni hayati Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndie aliyeuasisi. Kumbe unaweza kuthibitisha kuwa, chimbo la mwenge huo wa uhuru, ni maono ya Baba wa taifa, hasa pale alipousimamisha juu ya mlima Kilimanjaro. Akatamka kuwa, ‘ lengo ni kuleta matumaini pale pasipo na matumaini, upendo pale penye chuki na heshima pale palipojaa dharau’ . Mwenge huo, kwa mara ya kwanza, uliwashwa mwaka 1961, baada ya Mwalimu Nyerere kumteua Luteni Alexander Gwebe Nyirenda kutekeleza azma hiyo iliyoitwa “Operesheni Mwangaza”. Kwa mwaka jana, aliyekua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Philipi Isdori Mpango, wakati akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Pwani, kwenye uzinduzi, alisema mwenge ni kielelezo cha umoja na mshikamano. Akafafanua kuwa, tangu ...